Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU VIHATARISHI, DALILI NA MATIBABU YA UVIMBE KATIKA MJI WA MIMBA



UVUMBE KWENYE MJI WA MIMBA

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU VIHATARISHI, DALILI NA MATIBABU YA UVIMBE KATIKA MJI WA MIMBA 


Fibroids ni uvimbe usio wa saratani ambao hutokea kwenye misuli laini ya kuta za mji wa mimba. Ni miongoni mwa vimbe ambazo huwapata wanawake wengi. Vimbe hizi huanzia ktk moja ya seli ambayo hugawanyika na kutengeneza uvimbe. Homoni ya estrogen huchangia ukuaji wake. 


Uvimbe huu ni wa duara, mweupe mgumu na huweza kuwa mmoja au kuwa katika makundi.


VIHATARISHI

1. Kurithi

2. Umri (huwapata zaidi wanawake katika miaka 35-40)

3. Lishe

4. Uzito uliopitiliza

5. Kuchelewa kubeba mimba 

6. Unywaji pombe 

7. Kuvunja ungo katika umri mdogo

8. Matatizo ya tezi ya thyroid

9. Kisukari 

10. Kiwango kingi cha homoni ya estrogen


SABABU ZINAZOPUNGUZA HATARI YA KUPATA UVIMBE

1. Mazoezi

2. Kuwa na idadi kubwa ya nzao/watoto

3. Mboga za majani

4. Uvutaji wa sigara (sikushauri uvute sigara)


SABABU

1. Mabadiliko ya kigenetics

2. Homoni aina ya steroids ambazo hupelekea kugawanyika kwa seli.


DALILI

1. Maumivu makali wakati wa hedhi

2. Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

3. Ugumba

4. Kupata hedhi inayodumu zaidi ya siku saba au kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi

5. Hedhi zisizokuwa na mpangilio, kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi

6. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu

7. Maumivu ya nyonga

8. Tumbo kuongezeka

9. Kukosa choo, maumivu wakati wa kukojoa au kushindwa kukojoa

10. Upungufu wa damu


MADHARA YA UVIMBE WAKATI WA MIMBA

1. Kuharibika kwa mimba

2. Mlalo wa mtoto usio sahihi

3. Kuzaa kabla ya wakati

4. Kutokwa na damu nyingi mara baada ya kujifungua.


MATIBABU

Ikumbukwe kuwa asilimia 75 ya wanawake wenye uvimbe hawaoneshi dalili yoyote. Iwapo mtu atakuwa na dalili matibabu uhusisha

1. Dawa 

2. Upasuaji wa kutoa uvimbe au kutoa mji wa mimba

3. Kuziba kwa mishipa ya damu ili kuzuia damu isifikie uvimbe 


By Emmanuel Lwamayanga 

Afya ni kitu bora zaidi


.


 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!






Post a Comment

0 Comments