FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU ZA KUSHINDWA KUSIMAMISHA AU KUDUMISHA USIMAMAJI WA UUME ( ERECTILE DYSFUNCTION)

KUSHINDWA KUSIMAMISHA

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU ZA KUSHINDWA KUSIMAMISHA AU KUDUMISHA USIMAMAJI WA UUME ( ERECTILE DYSFUNCTION) 


Ili mwanaume aweze kushiriki tendo la ndoa anahitaji hamu ya tendo,  uwezo wa kusimamisha uume,  na uwezo wa kutengeneza na kutoa mbegu. Hamu ya tendo kwa mwanaume hutokana na kuona,  kusikia,  kunusa, kugusa, kufikiri na michocheo ya homoni.  Homoni ya testosterone uongeza hamu. 


Kusimama kwa uume hutegemea ongezeko la damu ktk mtandao wa mishipa na uwazi ktk uume ikiambatana na kulegea kwa kuta za mishipa ya ateri na misuli. Mfumo wa fahamu pia unamchango mkubwa juu ya hili. Nitric oxide ambayo huzalishwa mwilini inachochea usimamaji wa uume. 


TATIZO la kushindwa kusimamisha uume linapatikana zaidi kwa wanaume wenye matatizo kama kisukari, uzito uliopitiliza, matibabu ya saratani ya tezi dume kwa mionzi na upasuaji, magonjwa ya moyo, kupungua kwa cholesterol nzur mwilini, uvutaji wa sigara na matatizo ya ugwe mgongo. 


Kisukari,  matatizo ya mishipa ya damu na madhara ya dawa kwa pamoja ufanya 80% ya tatizo hili. 


NAMNA INAVYOTOKEA

tatizo hili huweza kutokana na

1. Kushindwa kuanzisha usimamaji (mfumo wa fahamu (kisaikolojia) na Homoni) 

2. Kushindwa kujaza mishipa ya damu

3. Kushindwa kuhifadhi damu kwenye uume

Makundi haya matatu hutegemeana


1. Mishipa ya damu

Miongoni mwa sababu kubwa ni tatizo la damu kufika au kutoka kwenye uume.  Matatizo ya mishipa kama kutuama kwa mafuta kwenye kuta zake hupelekea kupunguza kiwango cha damu kinachofikia uume na hivyo kushusha uimara lakin pia kutoka kwa damu ktk uume kurudi ktk mfumo wa mzunguko wa damu husababisha tatizo hili.  Mabadiliko ya kimaumbile ndan ya uume ni sababu pia


2. Mfumo wa fahamu

Ajari ktk ungwe mgongo na matatizo ktk mfumo wa fahamu 

3. Homoni

Kuongezeka kwa homoni ya prolactin na kupungua kwa homoni ya testosterone husababisha tatizo hili


4. Kisukari

Madhara ya kisukari ktk mishipa ya damu na mishipa ya fahamu lakini pia kiwango kidogo cha nitric oxide kwa wagonjwa hawa husababisha tatizo hili


5. Matatizo ya kisaikolojia

Uoga wa kushindwa kumlizisha mwenza, sonono, ugomvi/kutokuelewana, uoga aa mimba na magonjwa ya zinaa nk. 

6. Dawa

Baadhi ya dawa za presha

Na dawa za kulevya




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!