Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI, KUAMKA MARA KWA MARA USIKU, KUCHELEWA KUPATA USINGIZI AU KUSHINDWA KUPATA USINGIZI TENA MARA BAADA YA KUSHITUKA.



TATIZO LA KUKOSA USINGIZI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI, KUAMKA MARA KWA MARA USIKU, KUCHELEWA KUPATA USINGIZI AU KUSHINDWA KUPATA USINGIZI TENA MARA BAADA YA KUSHITUKA. 


SABABU ZA TATIZO HILI


1. SAIKOLOJIA NA FISIOLOJIA

watu wengi wenye tatizo hili wanamategemeo hasi ambayo huongeza wasiwasi na hivyo kupelekea ukosefu wa usingizi usiku. 


2. Kukosa utaratibu mzuri wa kulala.  Baadhi ya wagonjwa hujenga tabia ambazo hupelekea kukua kwa tatizo hili, 

1. Kulala mchana

2. Kutumia vitu kama tumbaku caffeine na kahawa muda mchache kabla ya kulala

3. Kugombana na wenza wao usiku kabla ya kulala

4. Kulala na simu (smartphones au tablets)  kitandani. 

5. Kufanyia kazi zao kitandani kama kusoma kuangalia tv au movie,  kula nk



3. Matatizo ya akili kama sonono

4. Dawa na dawa za kulevya. 

Baadhi ya dawa kama zile zitumikazo kutibu sonono,  kuacha ghafla matumizi ya pombe,  tumbaku caffeine nk huchangia tatizo hili.

 

5. Magonjwa katika mfumo wa upumuaji kama pumu,  maumivu,  magonjwa ya moyo nk humfanya mtu asipate usingizi na asiweze kulala usiku. 


6. Magonjwa katika mfumo wa fahamu. 

MATIBABU,. matibabu ya tatizo hili uhusisha saikolojia (ushauri na elimu juu ya tatizo husika)  pamoja na dawa.  Iwapo unatatizo hili fika katika kituo cha kutolea huduma upate kuhudumiwa. 

By Emmanuel Lwamayanga






Post a Comment

0 Comments