FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI, KUAMKA MARA KWA MARA USIKU, KUCHELEWA KUPATA USINGIZI AU KUSHINDWA KUPATA USINGIZI TENA MARA BAADA YA KUSHITUKA
USINGIZI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUKOSA USINGIZI, KUAMKA MARA KWA MARA USIKU, KUCHELEWA KUPATA USINGIZI AU KUSHINDWA KUPATA USINGIZI TENA MARA BAADA YA KUSHITUKA.
Iwapo mtu ana muda wa kutosha wengi ulala masaa 7-8 kwa usiku. Kupitia vipimo kama EEG, EOG na EMG usingizi umegawanywa katika hatua kuu 2 ambazo hufatana na hujirudia rudia katika kipindi chote mtu awapo usingizini.
1. Mwendo wa haraka wa macho
2. Mwendo husio haraka, hatua hii pia imegawanyika ktk hatua 3.
Umri unanafasi kubwa ktk mpangilio mzima wa usingizi.
Ukosefu wa usingizi huathiri utambuzi. Tafiti zinaonesha ukosefu wa usingizi huweza kusababisha kisukari, uzito uliopitiliza, kupungua kwa ufanyaji kazi wa kinga mwili, hatar za magonjwa ya moyo nk.
Swala la usingizi na kuwa macho linaendeshwa na ubongo. Iwapo kuna tatizo ktk sehemu husika basi mtu atapata tatizo. Baadhi ya seli za fahamu hupotea kadri umri unavyokwenda na hii hupelekea watu ambao umri umeenda kupata shida ktk kudumisha usingizi. Kuharibika kwa seli za fahamu zinazohusika na ile hatua ya mwendo wa haraka wa macho (REM) hupelekea watu kuigiza kile wanachokiota wakiwa usingizini.
Mtu anapokuwa macho kwa muda mrefu kiwango cha adenosine kinaongezeka ktk maeneo ya ubongo na hivyo adenosine huzuia yale maeneo yanayomfanya mtu awe macho na hivyo mtu huyo hupata usingizi. Prostaglandin D2 hufanya kazi sawa na adenosine.
INSOMNIA(kushindwa kuanzisha au kudumisha usingizi usiku). Watu wenye usingizi hafifu uhisi kuwa hali hii inawaathiri na kushusha utendaji kazi wao kazini na ktk jamii. Watu wenyr tatizo hili pia huhisi kuchoka, kupungua kwa mihemko na matatizo ktk utambuzi.
10% ya watu huwa na tatizo sugu linalodumu zaidi ya miezi 3. Huwapata zaidi wanawake, watu wazima/wazee, watu wa hali ya chin, wanaotumia madawa na wenye matatizo ya akili.
30% ya watu huwa na tatizo la muda mfupi, na huchangiwa na msongo wa mawazo(stress mbali mbali za maisha) kama kukosa kazi, magonjwa nk
Mara nyingi tatixo hili huanza ukubwani. Tafiti zinaonesha tatizo hili linaambatana na kuchochewa kwa sehemu za ubongo ambazo hufanya kazi mtu awapo macho.
By Emmanuel
Fuatilia mwendelezo wa somo hili ktk makala ijayo. Asante
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!