KUTEMBEA USINGIZINI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUTEMBEA USINGIZINI.
watu walioathirika na tatizo hili hufanya matendo mepesi mpaka magumu yanayohusisha misuli na mfumo husika wakiwa usingizini.
Matendo/matukio hayo ni kama kutembea, kukojoa, kula, kutoka nje ya nyumba na wengine hata kuendesha gari.
Baadhi yao iwapo watashituliwa au kuamshwa huwa wanakuwa ni wakali ja wenye fujo/vurugu sana.
Tatizo hili hutokea katika hatua ya usingizi ifahamikayo kama "mwendo wa haraka wa macho hatua ya tatu" kitaalamu (NREM stage N3 sleep) mara nyingi masaa machache ya mwanzo wakati wa usiku.
15% ya watoto huweza kupata tatizo hili na kati yao asilimia 1 hudumu mpaka ukubwani. Tendo hili huweza kutokea mara moja na kwa baadhi ya watoto hujirudia rudia mara baada ya matibabu.
Sababu haifahamiki japo kuwa theluthi moja ya wenye tatizo hili huonekana kurithi katika familia zao. Huchochewa zaidi na kukosa usingizi wa kutosha kwa muda mrefu, pombe na stress.
Familia zinatakiwa kuweka mazingira ya nyumba safi na salama ili kuzuia ajari iwapo mtu huyu atapatwa na tatizo hili.
By Emmanuel Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!