FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI (UKENI).
DAMU
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU SEHEMU ZA SIRI (UKENI).
katika hali ya kawaida mzunguko wa hedhi kwa wanawake wengi ni kati ya siku 21-35 na damu hii hudumu kwa siku 4-5 katika hali ya kawaida na wingi wake ni wastani wa mililita 35 (20-80mls). Kutokwa na damu ukweni si ugonjwa bali ni dalili ya tatizo jingine katika mwili.
Yako matatizo mengi yanayolikumba swala zima la hedhi. Tatizo hili huwapata wanawake wa umri wowote kuanzia watoto mpaka wazee waliofika ukomo wa hedhi. Baadhi ya wanawake huwa na mzunguko wa kawaida lakin mara zote mzunguko huo umekuwa wakitokwa na damu nyingi sana na hutokwa na damu zaid ya siku 7 mfululizo. Idadi kadhaa ya wanawake hutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi, na baadhi hutokwa na damu takriban mzunguko mzima. Kuna wanawake ambao mzunguko wao huzidi siku 35 na kuna wale ambao ni chini ya siku 21. Pia kuna asilimia ya wanawake hutokwa na damu mara baada ya kushiriki tendo la ndoa.
Kalenda ni moja ya njia zitumikazo kuchunguza/kugundua mabadiliko ktk mzunguko wa hedhi.
SABABU
sababu za kutokwa na damu ukeni kwa wingi au kwa muda mrefu zimegawanywa ktk makundi makuu sita.
1. Mabadiliko ya kimaumbile
2. Matatizo ya homoni
3. Maambukizi
4. Magonjwa katika sehemu mbalimbali za mwili
5. Madawa
6. Athari/ madhara/ changamoto za mimba.
Kutoka kwenye makundi hayo juu tunapata sababu kama
1. Uvimbe katika via vya uzazi
2. Kujipandikiza kwa tishu za ukuta wa ndani wa mji wa mimba ktk misuli ya mji huo
3. Saratani katika mji wa mimba
4. Matatizo katika mfumo wa ugandaji wa damu.
5. Mabadiliko ktk mzunguko wa hedhi yasababishwayo na homoni
6. Mimba (kuharibika, kujipandikiza nje ya mji wa mimba nk)
7. Baadhi ya vifaa vitumikavyo katika panga uzazi huweza kuwa chanzo
8. Kushindwa kwa figo na ini kufanya kazi yake lakini pia matatizo katika tezi mbalimbali ikiwemo pituitari na thyroidi.
JE UTAJUAJE KAMA UNATOKA DAMU NYINGI
Dalili za tatizo hili ni kama
1. Kutokwa na damu ya hedhi nyingi na/au kwa muda unaozidi siku saba.
2. Kutokwa na mabonge mabonge ya damu ukeni
3. Kuongezeka kwa idadi ya pedi au vipande vya kanga wakati wa hedhi
4. Kuwa na dalili za upungufu wa damu mwilini
by Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!