Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA MAUMIVU YA TUMBO KATIKA SIKU ZA HATARI ZA MWANAMKE. (MITTELSCHMERZ'S SYNDROME/ OVULAR PAIN)



MAUMIVU+TUMBO

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA MAUMIVU YA TUMBO KATIKA SIKU ZA HATARI ZA MWANAMKE. (MITTELSCHMERZ'S SYNDROME/ OVULAR PAIN) 


hali hii si tatizo la mara kwa mara na hutokea katikati ya mzunguko wa hedhi wa mwanamke.  Maumivu haya hupatikana katika sehemu ya chini ya tumbo chini ya kitovu na upande wa pembeni wa tumbo.  Mara nyingi maumivu haya hupatikana upande mmoja. 


Mara chache maumivu haya huweza kudumu kwa zaidi ya masaa 12. Na huweza kuambatana na kutokwa na kiwango kidogo cha damu ukeni au kutokwa na ute ute mwingi katika uke. 


SABABU


sababu kamili inayopelekea hali hii haifahamiki,  japo inasadikika kuwa yafuatayo yanaweza kuwa chanzo. 

1. Kuongezeka kwa msukumo katika sehemu iifadhiyo yai mara kabla ya kupasuka. 

2. Kugazabika kwa ukuta wa ndani wa tumbo kutokana na majimaji yapatikanayo baada ya kupevuka kwa yai. 

3. Kusinyaa/kujivuta/kukakamaa kwa mishipa na mji wa mimba. 


MATIBABU


Matibabu yake ni kupewa tu uhakika kuwa tatizo hili litaisha baada ya muda mfupi lakini pia ni pamoja na matumizi ya dawa za kutuliza maumivu iwapo tu kuna ulazima. 

Ikiwa tatizo hili linakusumbua,  mwone daktari kabla ya kutumia chochote kile. 

By Emmanuel Lwamayanga






Post a Comment

0 Comments