FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA MTINDIO WA UBONGO, SABABU, DALILI MATIBABU NA NJIA ZA KUZUIA(KUMKINGA MWANAO).
MTINDIO WA UBONGO
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA MTINDIO WA UBONGO, SABABU, DALILI MATIBABU NA NJIA ZA KUZUIA(KUMKINGA MWANAO).
Baadhi ya familia zimekuwa na imani potofu juu ya watoto wenye mtindio wa ubongo. Wengi wanaamini kuwa ni laana au mkosi kupata mtoto huyo. Hii inasababishwa na kukosekana kwa elimu katika jamii. Imani/dhana hii ni potofu.
Mtindio wa ubongo( cerebral palsy) nj tatizo linalokumba ubongo wa (mtoto mchanga) linaloathiri ukuaji au maendeleo ya misuli na hivyo kupelekea shida katika kutembea, uratibu au mkao wa mtu huyo. Tukio hili huukumba ubongo ambao bado haujakomaa.
Inasadikika kuwa tatizo hili linatokea kwa watoto 2 kati ya 1000 wanaozaliwa.
Shida katika misuli huambatana na matatizo katika tabia, utambuzi, mawasiliano, mitazamo na kifafa.
VISABABISHI VYA MTINDIO WA UBONGO
Sababu zinazopelekea mtu kupata mtindio wa ubongo zinaweza kuwepo wakati mtoto yuko tumboni, wakati wa kuzaliwa au baada ya kuzaliwa. Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu.
1. Kurithi
2. Mama kuwa na magonjwa wakati wa ujauzito( kwamfano homa na UTI)
3. Kupigwa na mionzi mikali kwa muda mrefu au kiwango kikubwa cha mionzi
4. Mtoto Kukosa hewa(oksijeni) akiwa tumboni au mara baada ya kuzaliwa
SABABU BAADA YA KUZALIWA KWA MTOTO
5. Magonjwa ya mfumo wa ufahamu wa mtoto
6. mtoto kuwa na kiwango kidogo cha sukari mwilini
7. Manjano
8. Ajari zinazopelekea kuvilia kwa damu kwenye ubongo
9. Kuzaliwa mtoto njiti humweka mtoto katika hatari ya kupata tatizo hili.
DALILI
Watoto wengi huonesha dalili kati ya miezi 4-12
1. Kutambaa kwa mguu mmoja
2. Kutumia upande mmoja wa mwili zaid ya upande mwingine.
3. Kutoka mate mdomon
4. Akisimama au kutembea huvuta mguu mmoja n.k
MATIBABU MUONE DAKTARI
(Matibabu ya mtindio wa ubongo huusisha vitengo mbalimbali kama daktari wa watoto, mtaalamu wa lishe, mama cheza, madaktari wa upasuaji n.k)
NJIA ZA KUMKINGA MWANAO ASIPATWE NA TATIZO HILI.
1. Chanjo kwa watoto wa kike
2. Kuwa na mahudhurio ya mara kwa mara mwanamke ushikapo mimba
3. Kupimwa kwa ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid
4. Kumwekea mazingira mazuri mtoto awapo nyumbani ili kuzuia ajari zinazoweza athiri kichwa
5. Kutibu ugonjwa wa manjano kikamilifu.
Tukiwapenda wataishi miaka mingi #kuzeeka
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!