FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA ENDOMETRIOSIS.

ENDOMETRIOSIS

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA ENDOMETRIOSIS. 


ENDOMETRIOSIS ni kuwapo kwa tishu/sehemu/nyama za ukuta wa ndani wa mji wa mimba katika sehemu nyingine ya mwili. (yaani tishu hizi zinajipandikiza nje ya ukuta wa ndani wa mji wa mimba) 


Mabadiliko ya homoni katika mzunguko huchangia ukuaji katika tishu hizi. 


Tishu hizi huweza kujipandikiza katika ovari,  sehemu za tumbo chini ya kitovu katika ogani mbalimbali,  misuli ya nyumba ya uzazi,  uke,  shingo ya kizazi,  mishipa ya fallopiani,  utumbo mpana,  kidole tumbo,  na sehemu nyingine nyingi. 


HUWAPATA WATU GANI? 


Kumekuwa na ongezeko la tatizo hili katika siku za hivi karibuni sababu ikiwa kuchelewa kuolewa,  kuchelewa kuzaa na kukua kwa sayansi na teknolojia na hivyo kusaidia kugundulika kwa tatizo hili hata kwa wale wasio na dalili. 


Tatizo hili huwapata wanawake wenye umri kati ya miaka 30-45, ambao hawajazaa au wenye mtoto mmoja au wawili na wamekaa muda mrefu sana pasipo kuzaa. 


SABABU, 

sababu ya tatizo hili bado haijawa wazi japo zipo dhana zinazoelezea tatizo hili nazo ni

1.  Kurudi nyuma kwa damu/ uchafu wa hedhi na hivyo kujipandikiza katika sehemu za juu katika nyonga

2. Damu/ uchafu wa hedhi kusababisha mabadiliko ya seli katika sehemu mbali mbali za njia ya uzazi na hivyo kuzifanya seli hizi kuwa kama seli zinazotengeneza sehemu ya ndani ya mji wa mimba

3. Kujipandikiza kwa moja kwa moja kwa tishu hizi

4.  Kurithi na mabadiliko yatokanayo na mazingira (sumu) 

5. Kusambaa kwa tishu hizi kwa njia ya damu au njia ya mfumo wa limfu. 

6. Kuziba kwa njia ya kawaida inayohusika na utoaji nje wa uchafu wa hedhi. 


DALILI

25% ya wanawake wenye tatizo hili hawaoneshi dalili. 

1. Maumivu makali ya nyonga na tumbo 

2. Maumivu wakati wa tendo la ndoa

3. Maumivu makali wakati wa hedhi

4. Kutokwa na damu kusiko kwa kawaida

5. Ugumba

6. Dalili nyingine zinategemeana na sehemu ilipojipandikiza tishu hiyo. 

MADHARA

1. Mabadiliko ya homoni

2. Maambukizi katika njia ya mkojo

3. Nk


MATIBABU 

kuna matibabu kwa njia ya dawa na kwa upasuaji.  By Emmanuel Lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!