MATEGE
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA MATEGE(RICKETS)
Kwa kawaida mifupa inatengenezwa na Mchanganyiko wa protini (osteoid) na madini kama calcium na phosphate. Kutokuwapo kwa madini haya kunapelekea mifupa kuwa laini na rahisi kuvunjika kwa watoto na hata watu wazima.
Matege ni tatizo linayoikumba mifupa inayokua na inasababishwa na kutokuwapo kwa madini hasa katika sehemu za mifupa zinazohusika na ukuaji kabla ukuaji haujafikia ukomo. Kutokuwepo kwa madini husababisha mifupa hii kuwa laini sana na hivyo kupinda kwa urahisi hasa kutokata na uzito wa mwili au nguvu ya mvutano itokanayo na misuli.
SABABU
1. kimsingi matege husababishwa na ukosefu wa vitamini D
2. Ukosefu wa madini aina ya calcium na phosphate
3. Matatizo katika figo
Kula vyakula vyenye upungufu wa vitamin D na madini husika, kutumia dawa zinazokinzana na calcium, kutumia dawa zenye aluminium kwa ajili ya kuzuia asidi na magonjwa ya figo yanayoongeza kiwango cha kutolewa kwa madini haya mwilini vyote vinapelekea tatizo hili.
DALILI
1. Kudumaa
2. Kujihisi huna nguvu na kutokuwa na hamu ya kufanya chochote
3. Tumbo kuongezeka ukubwa
4. Misuli kulegea na kukosa nguvu
5. Kuvunjika kwa mifupa
6. Dege dege
7. Kukakamaa
8. Kutoa kisauti wakati wa kupumua.
Katika kichwa dalili zake ni
1. Kulainika kwa mifupa ya kichwa
2. Komo la mbele kuongezeka
3. Kuchelewa kuota meno
4. Kuchelewa kufunga kwa uwazi wa kichwa
Kifuani
1. Maambukizi katika mfumo wa upumuaji
2. Kuvimba kwa kiunganishi kati ya sehemu ya mbavu na cartilage na hivyo kupangana kama chembe ya rozari
3. Kutokea kwa kishimo mwisho wa mbavu wakati wa kupumua
Mgongoni
1. Kupinda kwa sehemu mbalimbali za mgongo
Miguuni
1. Kuongezeka kwa upana wa vifundo vya miguu na mikono
2. Maumivu ya miguu
3. Matatizo katika nyonga
4. Kupinda kwa miguu
DAKTARI WAKO ATATAKA KUJUA YAFUATAYO
1. Aina ya vyakula unavyompa mwanao
2. Muda ambao mwanao anautumia akiwa nje (juani), aina ya mavazi anayovaa kwani jua linahusika katika utengenezaji wa vitamin D
3. Dawa anazotumia mtoto kwamfano matumizi ya dawa za degedege kunaongeza kuvunjwavunjwa kwa vitamin D na matumizi ya baadhi ya dawa zenye aluminium hupunguza kufyonzwa kwa phosphate
4. Matatizo ya figo.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!