FAHAMU KUHUSIANA NA TETENASI/PEPOPUNDA

TETENASI/PEPOPUNDA

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA TETENASI/PEPOPUNDA. 


TETENASI ni maambukizi ya papo hapo/ghafla yenye sifa bainifu ya mvutano/kukakamaa kwa misuli pamoja na shida ktk mfumo wa fahamu. 


SABABU


tatizo hili husababishwa na sumu kali itengenezwayo na bakteria wafahamikao kama clostridium tetani.  Bakteria hawa wanapatikana pahali kote duniani na hupatikana kwenye vumbi udongo nk. Bakteria hawa hutengeneza mbelewele/mbegu (spores)  ambazo zinauwezo wa kudumu kwa muda mrefu ktk mazingira na pia haziharibiwi kwa kemikali nyingi au kuchemshwa. Pia mbegu hizi hupatikana kwenye utumbo wa wanyama wengi na hivyo kufanya kinyesi kuwa moja ya njia ya kusambaa kwake.  


Mbelewele/mbegu hizi huingia mwilini kupitia jeraha litokanalo na mkwaruzo,  mchubuko au donda.  Kwa watoto wachanga huweza pitia kwenye kitovu hasa kwa zile jamii zenye desturi za kuweka kinyesi cha wanyama kwenye vitovu vya watoto wachanga. 


Iwapo matibabu hayatopatikana mapema matokeo ya ugonjwa huu ni makubwa na hata kifo. 


DALILI

1. maumivu makali ya misuli na kukakamaa

2. Maumivu ya mgongo

3. Shida katika kumeza

4. Kushindwa kunyonywa(mtoto mchanga) 

5. Joto kali

6. Mvutano wa misuli

7. Shinikizo la damu 

8. Mapigo ya moyo kwenda mbio

9. Kukosa choo

10. Kuongezeka makohozi

11. Figo kushindwa kufanya kazi ghafla. 

12. Kushindwa kupumua na kupaliwa. 

MATIBABU


TAFADHARI UONAPO DALILI AMA UPATAPO KIDONDA AU JERAHA KATIKA MAZINGIRA HATARISHI FIKA HOSPITALI MAPEMA,  KUCHELEWA KUPATA HUDUMA HUPELEKEA KIFO. 


NJIA ZA KUJIKINGA 


1. Usafi na utunzaji bora wa majeraha/vidonda

2. Kupata chanjo sahihi na kumaliza dozi ya chanjo sitahiki. Mama mjamzito hakikisha unapata chanjo,  hakikisha mwanao anapata chanjo nawe mtu mzima iwapo umepata tatizo/ajari/jeraha fika kituo kitoacho huduma mapema na kama utastahiri chanjo hakikisha unamaliza dozi. 

DALILI ZINAZOONESHA UWENDA MATOKEO YAKAWA MABAYA


1. Umri zaidi ya miaka 70

2. Shinikizo la juu la damu

3. Joto zaidi ya 38.5

4. Dalili kuonekana chini ya siku 7 toka kupatikana kwa jeraha. 

5. Dalili kuongezeka kwa kasi kubwa

6. Mapigo ya moyo zaid ya 140/m


Kwa maswali tuwasiliane DM 

Afya ni kitu bora zaidi 

By Emmanuel Lwamayanga.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!