FAHAMU KUHUSIANA NA UGONJWA WA AKILI (SCHIZOPHRENIA)

UGONJWA WA AKILI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA UGONJWA WA AKILI (SCHIZOPHRENIA)


Schizophrenia ni nini?

Hili ni kundi la magonjwa au matatizo ya kiakili ambayo hupelekea mabadiliko katika mitazamo, hisia, utambuzi, ufikiri na tabia.


Matatizo haya huanza kabla ya miaka 25 na huweza kudumu kwa kipindi chote cha uhai na huweza kumpata mtu yoyote bila kujali hali ya uchumi. Kutokuwapo kwa elimu juu ya tatizo hili kumewaweka wagonjwa hawa pamoja na ndugu zao katika hali ngumu katika jamii ikiwemo kutengwa.


Hakuna vipimo vya kimaabara vinavyoweza pima tatizo hili. Na asilimia 0.6-1.9 hupata tatizo hili katika kipindi chote cha uhai. Tatizo hili uwakumba wanaume na wanawake katika uwiano sawa.


SABABU

Uhusiano kati ya mazingira na jeni (genetics) inasadikika kuwa sababu ya kutokea kwa tatizo hili. Lakini pia kuongezeka kwa ufanyaji kazi wa kemikali zifahamikazo kama dopamine pamoja na serotonin vinahusishwa katika hili.


VIHATARISHI 

1. Matatizo katika mfumo wa neva unaohusika na uchakataji akili

2. Dawa na madawa ya kulevya kama bangi

3. Ukosefu wa oksijen kwa kichanga kiwapo tumboni

4. Maambukizi

5. Mama kukosa virutubisho akiwa mjamzito

6. Kuwa na ndugu wa karibu mwenye tatizo hili. 


DALILI

1. Kuona vitu au watu ama kusikia sauti zisizokuwepo au zisizosikiwa na watu wengine

2. Kuwa na fikra za ajabu

3. Kuwa na uoga au wasiwasi kuwa kina mtu anataka kukudhuru

4. Kujitenga

5. Kukosa motisha

6. Ukosefu wa uwezo wa kuhisi furaha na kutokuwa na hamu ya kuwa na mahusiano

7. Imani kuwa kuna nguvu za nje zinazoongoza mtu, kutoa au kuweka mawazo katika akili ya mtu au kusambaza mawazo ya mtu huyo kwa watu wengine

8. Uwezo duni wa kuzungumza

9. Maneno na fikra zao kukosa mpangilio

10. Kutokuzingatia usafi na kuvaa ovyo.


MATIBABU

Moja ya mambo muhimu ya kuzingatia ni kuwa karibu kuwapa sapoti watu wenye tatizo hili. Matatibabu yake uhusisha therapi ya akili pamoja na dawa zinazodhibiti uchakataji wa kemikali aina ya dopamine na serotonin. Matibabu hutumika kutibu dalili kuu za tatizo hili.


Afya ni kitu bora zaidi


By Emmanuel Lwamayanga

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!