FAHAMU KUHUSIANA NA UZAZI PINGAMIZI

UZAZI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA UZAZI PINGAMIZI


UZAZI PINGAMIZI NI NINI?


Huu  ni uzazi ambao licha ya kuwepo kwa uchungu wa kutosha mtoto anashindwa kushuka/kupita kwenye njia ya uzazi. Yaani inakuwa ni ngumu kuzaa kupitia njia ya kawaida.


Hali hii inawezasababishwa na matatizo kwenye njia ya uzazi au mtoto mwenyewe.


Uzazi pingamizi ni miongoni mwa sababu kubwa zinazosababisha vifo vya kinamama hasa katika nchi zinazoendelea.


Kutokana na ongezeko la mimba za utotoni, uzazi pingamizi umekuwa ukiongezeka katika nchi zinazoendelea.


SABABU ZINAZOPELEKEA UZAZI PINGAMIZI

Matatizo katika njia ya uzazi,

1. Kutokuwiana kwa nyonga na mtoto au kuwa na nyonga yenye shida

2. Uvimbe katika shingo ya kizazi au katika ligamenti

3. Makovu kwenye njia ya uzazi yatokanayo na upasuaji


Matatizo kwa mtoto 

1. Mlalo mbaya tumboni

2. Kutanguliza uso wakati wa kuzaliwa

3. Mtoto kuwa mkubwa (big baby)

4. Mtoto kutanguliza kichwa na kiungo kingine kama mkono wakati wa kuzaliwa

5. Mapacha walioungana


DALILI ZA UZAZI PINGAMIZI

Kwa mtu wa kawaida inawezekana asizigundue dalili hizi hivyo kina mama wote wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kuondokana na madhara yatokanayo na uzazi pingamizi.

1. Kutengenezeka kwa mkanda unaotenganisha sehemu ya juu na ya chini ya mji wa mimba(retraction or bandl’s ring)

2. Kukojoa mkojo wenye damu

3. Kuvimba sana kwa sehemu ya nje ya uke


MADHARA YA UZAZI PINGAMIZI


KWA MAMA

1. Kuchoka kutokana na kusukuma pasipo mafanikio

2. Kupungua kwa kiwango cha maji mwilini

3. Kuongezeka kwa kiwango cha asidi mwilini

4. Maambukizi katika njia/mfumo wa uzazi wa mwanamke

5. KUPASUKA KWA MJI WA MIMBA

6. Kutokwa na damu nyingi mara baada ya kujifungua

7. KUPATA FISTULA


MADHARA YA MIMBA PINGAMIZI KWA MTOTO

1. Mtoto kukosa okisijeni ya kutosha halii hii inaweza pelekea shida katika maendeleo ya ukuaji katika mfumo wa fahamu na mifumo mingine katika mwili

2. Kuvujia kwa damu kichwani

3. Maambukizi

4. Kifo


JINSI YA KUJIKINGA NA UZAZI PINGAMIZI

1. Zuia mimba za utotoni

2. Wanawake wote wajawazito wawe na maudhulio mazuri kliniki ili kugundua kama wapo katika hatari ya kupata uzazi pingamizi na hivyo kufanya maandalizi kwa ajili ya kujifungua.

3.Lishe wakati wa utotoni

By lwamayang




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!