FAHAMU KUHUSU KELOIDS.

KELOIDS

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU KELOIDS.


Keloids ni kuongezeka kulikopitiliza au kuvimba kwa tishu au nyama katika kovu. Kwa kiswahili rahisi keloids ni kovu lililovimba. 

Japokuwa keloids hazina madhara kiafya, zimekuwa zikiambatanishwa na matatizo ya kimuonekano na kisaikolojia.


Keloids zinaweza kuwa ngumu au laini. Mara nyingi hutokea kwenye kovu penyewe na husambaa na kuhusisha hata sehemu ambayo haikuwa na ajari hapo awali.


Keloids hupatikana kwenye maeneo kama kwene masikio, kifuani, shingo mabega na sehemu ya juu ya mgongo. Keloids hukuwa taratibu ndani ya miezi mpaka miaka. 

Imeonekana kuwa keloids zinakuwa haraka wakati wa barehe, mimba au kwa watu wenye matatizo ya tezi ya thyroid. Hali zote hizi huambatana na kuongezeka kwa homoni ambayo huusika katika kutokea kwa keloids.


SABABU

Japokuwa kuna asilimia kadhaa ya keloids ambazo hutokea pasipo sababu na mara nyingi huwapata wale ambao ndugu zao wanazo.

Zifuatazo ni baadhi ya asababu zinazopelekea kutokea kwa keloids.

1. Ajari- mara nyingi makovu hayahutokana na ajari kama michubuko, mikwaruzo, kutoboa masikio.

2. Kuungua

3. Mvuto wa ngozi (skin tension)

4. Maambukizi (makovu yatokanayo na tetekuwanga)

5. Hupungufu wa metalloproitenases. Kutokana na uwepo mdogo wa melanocytes kwenye viganja na unyayo kunapelekea kutokuwapo kwa keloids katika maeneo haya.

6. Baadhi ya wachunguzi wanahusisha kiwango kikubwa cha calcium mwilini na kutokea kwa keloids.


DALILI

Miongoni mwa dalili ni

1. Uvimbe

2. Kuwashwa kwenye kovu


MATIBABU:

Japokuwa keloids hazina madhara, watu wengi wamekuwa wakitaka ziondolewe ili kuleta muonekano mzuri katika miili yao.

Baadhi ya keloids huweza kunywea zenyewe na kupotea nyingine huitaji dawa ambazo huzifanya zinywee na kupotea kabisa na baadhi hutolewa kwa upasuaji.


By Emmanuel Lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!