Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KUHUSU KORODANI AMBAYO HAIJASHUKA KWENYE MFUKO WAKE WA KORODANI (undescended testis)



KORODANI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU KORODANI AMBAYO HAIJASHUKA KWENYE MFUKO WAKE WA KORODANI (undescended testis)


Hii ni tatizo linalotokea baada ya korodni kushindwa kuendelea na safari yake kuelekea kwenye mfuko wa korodani. 

Tatizo hili linapatikana kwenye asilimia 20-30% ya watoto njiti na asilimia 3% ya watoto waliotimiza siku zao. Tatizo hili lipo zaidi kwa watoto njiti kwasababu korodani hushuka kwenye mfuko wake katika miezi mitatu ya mwisho ya mimba.


75% ya watoto wenye tatizo hili korodan zao hushuka ndani ya miezi mitatu na ifikapo mwaka mmoja ni asilimia moja tu ya watoto ndio huwa na hili tatizo.


Kwa baadhi ya watoto tatizo hili hugundulika baadae sana.  Tatizo hili hutokea zaidi kwenye korodani ya upande wa kulia na 20% hutokea kwenye korodani zote mbili. 

Korodani hizi hubaki tumboni, shingo ya mfuko wa korodani au sehemu yoyote nje ya mfuko huo. Iwapo korodani itaendelea kuwa tumboni au sehemu nyingine nje ya mfuko wa korodani joto lililo katika maeneo haya hupelekea mabadiliko ikiwemo kupotea kwa seli za leydig na sertoli na kupungua kwa utengenezaji wa mbegu za kiume.


SABABU ZINAZOPELEKEA KORODANI ZISISHUKE.

Katika asilimia kubwa hakuna sababu ambayo imegundulika. Lakini matatizo ya homoni yamechangia katika kiwango kidogo cha tatizo hili.


Mara kadhaa wazazi wamekuwa wakieleza kuwa wamekuwa wakiona korodani za watoto wao  wakati wakiwaosha na kutokuziona tena wakati wa baridi.


DALILI 

Kushindwa kuzishika korodani kwenye mfuko wake au kushindwa kuzirudisha kwa njia ya kushikashika au kukamua. 

MADHARA YA KORODANI ZILIZOSHINDWA KUSHUKA.

1. Ugumba

2. Ngiri

3. Saratani

4. Kujisokota kwa korodani


MATIBABU 

Watoto wenye tatizo hili hutakiwa kutibiwa kabla hawajatimiza mwaka mmoja ili kupata matokeo chanya lakini pia kuzuia madhara yatokanayo na tatizo hili yaani ugumba na saratani. Matibabu yanaweza fanyika kwa dawa ambayo hutengenezwa kwa homoni kama hakutokuwa na maendeleo baada ya kutumia dawa upasuaji hufanyika.


By Emmanuel Lwamayanga






Post a Comment

0 Comments