PID
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU MAAMBUKIZI KATIKA MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE (PID)
PID ni nini?
Huu ni ugonjwa unaotokana na maambukizi katika sehemu ya juu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yaani (shingo ya kizazi, nyama ya ndani ya mji wa mimba, mji wa mimba wenyewe na mishipa ya falopio)
SABABU,
PID husababishwa na vijidudu/vimelea vya aina mbalimbali miongoni mwao ni vile visababishavyo kisonono kitaalamu huitwa (N. Gonorrhea) na vingine ni C. Trachomatis. Inaaminika kuwa vimelea hivi hupanda kutoka sehemu ya chini ya mfumo wa uzazi yaani uke kisha upita katika shingo ya kizazi na kuleta shida.
VISABABISHI/VIHATARISHI
1. Kuwa na umri mdogo
2. Kuwa na wapenzi wengi
3. Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya zinaa
4. Kujamiiana katika umri mdogo
5. Kufanya mapenzi wakati wa hedhi
6. Kujisafisha ukeni kwa kutumia maji mengi, sabuni, viungo au vitu visivyostahiki(vaginal douching) Hali hii uondoa uteute ambao ndio kinga ya kuzuia vijidudu kupanda, lakini pia kitendo hiki kinaweza kuwa ni njia ya kuingiza vijidudu katika mfumo wa uzazi
7. Hali duni ya kiuchumi
8. Kuingizwa vifaa ukeni(vipandikizi ndani ya mji wa mimba(lupu) au wakati wa kutoa mimba isivyo kitaalamu)
DALILI ZA PID
1. Maumivu makali ya tumbo hasa chini ya kitovu, kiuno, nyonga au mgongo
2. Kutokwa na uchafu wa njano na wenye harufu sehemu za siri
3. Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi au kutokwa na damu sehemu za siri pasipo na mpangilio
4. Homa
5. Maumivu wakati wa hedhi
6. Maumivu wakati wa tendo la ndoa/kujamiiana.
7. Homa, kichefuchefu kutapika na kuharisha
Ikumbukwe kuwa dalili hizi pia zinaweza kusababishwa na magonjwa mengine hivyo ni vyema kufika hospitali uonapo dalili hizi.
MADHARA YA PID
1. Ugumba
2. Mimba kutungwa nje ya mji wa mimba
3. Maumivu ya tumbo ya kudumu
4. Kutapakaa kwa vijidudu katika sehemu nyingine za mwili
5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Kushikamana/kugandana kwa sehemu mbalimbali za mwili
NJIA ZA KUZUIA
1. Kufanya ngono salama
2. Kutumia njia za uzazi wa mpango.
MATIBABU YA PID
Matibabu ya ugonjwa huu huusihswa dawa mbalimbali zinazouwa vijidudu. Hivyo uonapo dalili tajwa hapo juu fika hospitali ili kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu.
By Emmanuel Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!