FAHAMU KUHUSU MIMBA ILIYOTUNGWA NJE YA TUMBO LA UZAZI, vVISABABISHI DALILI NA MATIBABU YAKE.

MIMBA

• • • • • •


FAHAMU KUHUSU MIMBA ILIYOTUNGWA NJE YA TUMBO LA UZAZI, vVISABABISHI DALILI NA MATIBABU YAKE.


Baada ya urutubishwaji na ikiwa mshipa wa falopio ni mzima, matokeo ya urutubishwaji wa yai na mbegu za kiume(blastocytes) ujipandikiza kwenye ukuta wa ndani wa mji wa mimba(uterus) lakini asilimia chache(1-2%) ya mimba hutungwa au kupandikizwa nje ya mji/mfuko wa mimba, hali hii hufahamika kama mimba iliyotungwa nje ya tumbo la uzazi (yaani ECTOPIC PREGNANCY). Hali hii inasadikika kusababisha asilimia sita ya vifo vya mama wajawazito, lakini pia hupunguza uwezekano wa kubeba mimba ndani ya tumbo la uzazi.


Karibu 95% ya mimba zote zitungwazo nje ya mji/mfuko wa uzazi hutungwa katika sehemu tofauti tofauti za mshipa wa falopio na asilimia tano zilizobaki hutungwa kwenye ovali, tumboni, kwenye shingo ya kizazi na kwenye jeraha la upasuaji. Kuna baadhi ya mimba za mapacha ambazo pacha mmoja anakuwa kwenye tumbo la uzazi na mwingine anakuwa nje ya tumbo la uzazi.


VIHATARISHI/VISABABISHI

1. Mfumo mbaya/mbovu wa mshipa wa falopio

2. Upasuaji wa kutoa mimba iliyotungwa nje ya tumbo la uzazi

3. Kuwa na historia ya mimba kutungwa nje ya tumbo la uzazi kunaongeza uwezekano wa kupata mimba nyingine ambayo pia itakuwa nje

4. Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya zinaa au mahonjwa mengine yanayodhuru mfumo mzima wa uzazi

5. Kemikali kama diesthylstilbestrol ikiwa mama atakuwa kwenye mazingira hayo au matumizi yake ili hali ana mimba kemikali hii itamfanya mtoto alie tumboni kutokuimarika vizur katika mfumo wake wa uzazi hasa mshipa wa falopio.

6. Uvutaji wa tumbaku/sigara

7. Kubeba mimba katika Umri mkubwa (35-44)

8. Wapenzi wengi na kukutana kimwili na wanaume ikiwa una umri mdogo

9. Kushindwa kwa vitanzi kuzuia mimba(intrauterine devices) umuweka mama katika hatari ya kupata mimba nje ya tumbo la uzazi.


MATOKEO YA MIMBA ILIYOTUNGWA NJE YA TUMBO LA UZAZI.

1. Kupasuka kwa mshipa wa falopio

2. Mimba kutoka/kuharibika

3. Kushindwa kuendelea kwa mimba na kupotelea mwilini.



Mara nyingi kupasuka kwa mshipa wa falopio ambao umebeba mimba hutokea pasipo kuwa na sababu yoyote lakini kujamiiana na kufanyiwa baadhi ya vipimo kunaweza pelekea kupasuka.


DALILI

1. Kuchelewa/ kutokuingia hedhi

2. Maumivu makali

3. Kutokwa ba damu sehemu za siri

Iwapo mshipa wa falopio ukipasuka kutakuwa na 

1. Maumivu makali sana ya tumbo na kiuno. Maumivu haya huwa kama mtu amechomwa na kitu chenye ncha kali au amechanwa na kitu

2. Maumivu baada ya kuguswa au kushikwa tumbo(tenderness)

3. Uvimbe katika upande mmoja wa mji wa mimba

4. Maumivu ya shingo au bega hasa hasa pale unapovuta hewa ndani.

5. Kushuka kwa mapigo ya moyo

6. Kizunguzungu na kuzirahi

7. Shinikizo la chini la damu


MATIBABU

1. Dawa


2. Upasuaji.


Imeandaliwa na EMMANUEL LWAMAYANGA





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!