FAHAMU KUHUSU SABABU ZINAZOPELEKEA MDOMO KUWA MKAVU
MDOMO MKAVU
• • • •
FAHAMU KUHUSU SABABU ZINAZOPELEKEA KINYWA KUWA KIKAVU.
Tunafahamu kuwa mate yanakazi kubwa sana kinywani, ikiwemo kusaidia katika mmeng’enyo wa chakula, kuongea lakini pia kusafisha kinywa na hivyo kutukinga na baadhi ya vijidudu au mabaki ya chakula ambayo kwa njia moja au nyingine huweza pelekea shida mbali mbali za kinywa.
Watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa vinywa vyao ni vikavu na baadhibyao wamekuwa wakipata hata vidonda ndani na maeneo mengine kuzunguka kinywa, wamekuwa wakipata shida ya kumeza na hata kuongea, lakini ni asilimia chache kati yao ndio waliogundulika kuwa na shida katika utengenezaji wa mate yaani uwezo wa utengenezaji, au utoaji mate wa tezi za mate unakuwa umepungua, waliobaki ambao wao mfumo wa utengenezaji na utoaji mate uko sawa sababu ya wao kujisikia kinywa kikavu haijafahamika sawasawa.
SABABU
Miongoni mwa sababu zinazopelekea mtu kuhisi kinywa kikavu, sababu zinazopelekea kupungua kwa utengenezaji wa mate ni kama zifuatazo,
1. Kutokuwepo, kupotea au kupungua kwa tezi zinazotengeneza mate kunapelekea kupungua kwa utengenezaji wa mate. Tatizo hili mara nyingi mtu huzaliwa nalo japo kuwa sio kawaida mtu kukosa kabisa tezi hizi
2. Maambukizi, virusi aina ya paramyxovirus na aina mbalimbali za bakteria wanehusishwa katika kushambulia tezi hizi za mate na hivyo kuzuia utengenezaji wa mate
3. Kufuatia upasuaji, upungufu wa maji kufuatia upasuaji, lakini pia kutokuwepo kwa mrejesho wa maji hayo kunaweza pelekea tatizo hili
4. Kuvimba kwa tezi za mate
5. Saratani
6. Mionzi
7. Kuziba kwa mishipa ipitishayo mate
8. Uwoga au kupanic
9. Baadhi ya madawa, kinywa kikavu inaweza kuwa ni miongoni mwa madhara ya dawa mbalimbali
10. Upungufu wa vitamini
11. Kisukari
12. Upungufu wa utendaji kazi wa tezi ya throid
13. Upungufu wa damu mwilini n.k
MATIBABU
Fika kwa dakatari ili aweze gundua chanzo cha tatizo , lakini pia unaweza jitahidi kusafisha kinywa mara kwa mara kwa maji ili kulainisha mdomo, tafuna kitu kama “jojo” ili kuufanya mdomo uloane, na iwapo sababu ni dawa daktari atakwambia nini cha kufanya.
Kumbuka mdomo mkavu huweza pelekea hata kunuka kinywa, kuoza meno na shida nyingine nyingi hivyo muone daktari
By Emmanuel Lwamayanga.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!