SEKENENE
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU SEKENENE/ SEKELA (CHALAZION)
Kumekuwa na iman tofaut tofauti juu ya ugonjwa huu. Baadhi ya jamii wanaamin kuwa ugonjwa huu hupatikana endapo utamcheka mkwe au endapo utamcheka yule ambaye tayar anaugonjwa huu na baadhi wanaamin matibabu yake ni kuchungulia tundu la choo.
Kwa upande wa sayansi iko hivi
Sekela/ chalazion - ni kuvimba kusiko kwa tezi ya meibomian kusiko kwa maambukizi. Ubimbe huu hutokea kwenye sehemu ya nje ya jicho ishikiriayo kope.
VISABABISHI
1. Umri- sekela/sekenene hupata watu wenye umri wowote ikiwemo watoto vijana na hata wazee
2. Tabia ya kijifuta futa macho na pua kwa vidole
3. Kisukari
4. Ulaji mkubwa wa wanga
5. Unywaji wa pombe
NI KWA NAMNA GANI HALI HII HUTOKEA?
Sekela/ sekenene au chalazion huanza na maambukizi madogi katika tezi ya meibomian. Maambukizi haya husababishwa na vijidudu wasiokuwa na nguvu. Baada ya kuambukizwa hupelekea uenezi na uingiliaji wa seli za epithelia kwenye kuta za kifereji na hii hupelekea kuziba kwa kifereji hiki. Kuziba huku kusababisha kukusanyika kwa usiri/majimaji/sebum kwenye tezi hiyi na hivyo kusababisha kuvimba/kuongeZeka ukubwa. Sebum pia hushawishikuvimba zaid kwa tezi husika na sehemu za jiran.
DALILI
1. Uvimbe usio na maumivu jichoni
2. Kusikia uzito jichoni
3. Uono hafifu
4. Kutokwa na machozi
MATOKEO/MADHARA
Asilimia chache sana ya vimbe hizi huisha zenyewe pasipo hata matibabu. Vimbe nyingi huongezeka ukubwa na kuwa kubwa zaidi. Nyingine hupata maambukizi na nyingine huweza badilika kuwa saratani hasa kwa wazee.
MATIBABU
uonapo dalili fika kituo cha afya.
By Lwamayanga Emmanuel
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!