FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KUNUKA KINYWA(MDOMO) NA NJIA ZA KUZUIA
MDOMO
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KUNUKA KINYWA(MDOMO) NA NJIA ZA KUZUIA.
Tatizo sugu la kunuka kinywa humfanya mtu apate msongo wa mawazo lakini pia tatizo hili huweza kuharibu mahusiano ya mtu huyo na mwenza wake, ndugu jamaa rafiki na hata wafanyakazi wake.
NINI CHANZO CHA TATIZO SUGU LA KUNUKA KINYWA?
1. Sababu kubwa ya kunuka mdomo(kinywa) ni kukosa unadhifu wa kinywa. Watu wengi hawana tamaduni ya kusafisha kinywa na kwa baadhi ya wenye hiyo kawaida hufanya kwa mazoea hii upelekea kutuama kwa vyakula na wadudu na hivyo kunuka kinywa.
2. Matatizo ya meno kama meno kutoboka na kuwa na vishimo ndani ya kinywa hujenga mazingira ya wadudu wasababishao harufu mbaya kukua na kuzaliana.
3. Magonjwa ya sikio, pua na koo. Baadhi ya magonjwa haya upelekea utengenezwaji wa ute mzito(makamasi) ambayo yanapovutwa au kumezwa huwapa wadudu wasababishao harufu mbaya mazingira mazuri ya kuwasiliana.
4. Mdomo mkavu- mate yanafaida nyingi kwa kinywa ikiwemo kusaidia mmeng’enyo wa chakula, kusafisha kinywa lakini pia utengenezaji wa kinga dhidi ya wadudu. Mdomo mkavu husababishwa na madawa, magonjwa, matumizi ya pombe, tumbaku n.k
5. Uvutaji wa tumbaku(sigara)- huacha harufu ya aina yake mdomon ambayo hukaa kwa muda mrefu na ambayo haiondoki kwa njia za kawaida. Watumiaji wa tumbaki pia wapo katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya fizi ambayo pia hupelekea kunuka kwa kinywa.
6. Kutokula au kula vyakula visvyo na wanga hupelekea kuvunjwavunjwa kwa mafuta mwilini hali hii hupelekea kutengenezwa kwa ketones ambazo huwa na harufu kali.
7. Mabaki ya chakula mdomoni husaidia ukuaji wa wadudu ambao hutengeneza sulfur ambayo hupelekea kunuka kwa mdomo. Lakini pia matumizi ya viungo kama vitunguu swaumu, tangawizi na vyakula vyenye viungo vikali baada ya kumeng’enywa hufyonzwa na kuingia kwenye damu na hii hufikia kwenye mapafu na mtu huanza kutoa hewa yenye harufu mbaya.
8. Kunuka kinywa inaweza kuwa ni matokeo ya ugonjwa mwingine mkubwa katika sehemu nyingine ya mwilini kama ini, figo, kisukari na magonjwa ya mfumo wa upumuaji.
MATIBABU.
1. Safisha kinywa kila baada ya kula
2. Kunywa maji mengi
3. Punguza matumizi ya tumbaku
4. Kama tatizo limekuwa sugu MUONE DAKTARI.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!