FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU PUANI.

DAMU PUANI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU PUANI.


Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya watu duniani hupatwa na tatizo la kutokwa na damu puani walau mara moja katika kipindi chote cha maisha yao. Ziko sababu nyingi ambazo hupelekea tatizo hili ikiwemo ajari. Kutokwa na damu puani inaweza kuwa pia ni matokeo ya ugonjwa mwingine katika mifumo mbalimbali ya mwili.


Kwa asilimia kubwa ya watu sababu ya kutokwa na damu puani haifahamiki. 

Miongoni mwa hatua za awali katika huduma ya kwanza ni mgonjwa kuziba pua yake kwa kushika sehemu ya chini kwa muda wa dakika 20  kisha kuinamia mbele. Hii itazuia damu kurudi ndani na hivyo kumezwa.


Ni muhimu kutambua eneo linalotoa damu katika pua lakini pia kujua sababu ya kutokwa na damu puani, hii itasaidia katika kuzuia damu lakini pia kutibu tatizo.


MIONGONI MWA SABABU NI,

1. Ajari zisababishwazo na kujiumiza kwa kidole wakati wa kutoa makamasi yaliyoganda puani, kuingiza vitu visivyohitajika puani kama kalamu au mbegu za matunda kwa watoto wadogo, kuvunjika kwa sehemu za pua ikiwemo mifupa

2. Maambukizi katika pua

3. Moshi

4. Kemikali

5. Upasuaji puani

6. Saratani au vimbe katika maeneno tofauti tofauti ya pua

7. Kutoboka kwa sehemu za pua 

8. Baadhi ya dawa na madawa ya kulevya

9. Magonjwa kama - shinikizo la damu, saratani ya damu, magonjwabyanayozuia damu kuganda, upungufu wa viini damu vinavyosaidia damu kuganda.


MATIBABU

Mbali ya kuwa matibabu yake hutegemea zaidi kujua chanzo cha tatizo, matibabu haya uhusisha kuongezwa damu iwapo imepungua sana, kuharibu tishu kwa joto, ufungashaji wa pua na upasuaji unaohusisha kuziba kwa mishipa ya damu husika.


Baadhi ya dawa zimehusishwa pia katika kutibu tatizo hili na baadhi ya jamii wanatumia maji ya uvuguvugu kutibu tatizo la kutokwa na damu puani. Angaliazo hakikisha maji sik ya moto kwani iwapo maji yana joto zaidi ya nyuzi joto 50 yanaweza pelekea kutanuka kwa mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiwango cha damu kinachotoka puani.


Ni vyema ukamuona daktari ili kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha tatizo hilo.


By Emmanuel Lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!