FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA KUKOJOA KITANDANI.
KUKOJOA KITANDANI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA KUKOJOA KITANDANI.
Kukojoa kitandani ni ugonjwa ambao umeambatanishwa na vitendo kama unyanyapaaji na matatizo ya kisaikolojia katika jamii zetu. Swala la kukojoa kitandani ni la kawaida kwa watoto chini ya umri mitano. Ikiwa kitendo hiki kitazidi miaka mitano basi hilo ni tatizo.
Wazazi wengi wamekuwa wakiwahukumu watoto wao kwa kosa la kukojoa kitandani bila kujua kuwa tatizo hilo liko nje ya uwezo wa mtoto.
Kuna aina kuu mbili za tatizo hili
1. Aina ya kwanza inahusisha mtoto ambae hajawah kupata uwezo wa kuzuia kabisa mkojo kabisa tangu azaliwe
2. Aina ya pili ni watoto ambao awali walikuwa na uwezo wa kuzuia mkojo wakati wa usiku lakini ghafla wamepata tatizo hilo kwa muda wa miezi 6 au zaidi.
Inasadikika kuwa tatizo hili linawakumba zaidi ya 15% ya watoto. Na watoto wa kiume wanaathirika zaidi ikilinganishwa na watoto wa kike.
KWANINI HALI HII INATOKEA?
Kuna sababu kuu tatu ambazo zinahusika katika tatizo hili
1. Utengenezwaji wa mkojo mwingi sana wakati wa usiku
2. Kibofu kufanya kazi pasipokuwa na mpangilio au kufanya shughuli kupita kiasi
3. Kushindwa kuamka usiku iwapo kibofu kitajaa.
Mfumo wa fahamu umehusishwa pia kama moja ya sababu zinazopelekea tatizo hili. Matatizo au masumbuko katika usingizi kama kutembea usingizini yanaweza pelekea kutoweka kwa vichocheo zuizi katika kibofu na hivyo kusababisha kujikojolea wakati wa usiku.
VIHATARISHI
1. Matatizo katika mfumo wa fahamu
2. Matatizo katika uti wa mgongo
3. Msongo wa mawazo
4. Maambukizi katika mfumo wa mkojo
5. Kurithi/ kuwa na ndugu mwenye tatizo hili katika familia
6. Matatizo katika ukuaji
7. Kisukari
8. Matatizo ya kimaumbile
9. Maambukizi yasababishwayo na minyoo
10. Kuongezeka kwa ukinzani katika koo la hewa wakati wa usiku hali inayopelekea kukoroma
11. Kibofu kidogo
12. Matatizo yanayohusisha chromosome 8, 12, 13 na 22
13. Hali ya kutokupata choo
MADHARA
1. Athari kisaikolojia
2. Mchubuko wa ngozi kutokana na mkojo
MATIBABU
1. Kutumia kengere za kumuamsha mtoto ili akojoe
2. Kutumia dawa zinazoongeza ufyonzwaji wa maji kwenye mfumo wa mkojo na hivyo kupunguza kiwango cha mkojo kinachotengenezwa
3. Dawa zifanyazo kazi katika mfumo wa fahamu.
By Emma
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!