MATENDE
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA MATENDE, SABABU, DALILI NA MATIBABU.
Matende ni ugonjwa ambao huathiri mfumo wa limfu(lymphatic system) ambao ni mfumo wa ziada wa damu lakini pia ni mfumo wa kinga katika mwili.
Zaidi ya mamilioni ya watu katika nchi za kitropiki wanaishi katika mazingira hatarishi ya kupata ugonjwa huu. Japo kuwa sio ugonjwa unaopatikana sana lakini upo na watu wanapata.
Ugonjwa huu husambaza na mbu wa aina mbali mbali. Miongoni mwao ni mbu aina ya culex, anopheles na aedes.
Mara nyingi maambukizi haya hupatikana utotoni na vimelea hujificha na kuharibu mfumo huo wa limfu.
Japo kuwa muathirika hapati ulemevu wa kudumu, ugonjwa huu hupelekea matatizo ya kisaikolojia, kiuchumi na kijamii. baadhi ya jamii wamekuwa wakiwatenga kabisa wagonjwa hawa.
SABABU ZA UGONJWA WA MATENDE.
Matende husababishwa na maambukizi ya minyoo wapatikanao katika familia ya minyoo ifahamikayo kitaalamu kama Filariodidea. Kuna aina tatu za minyoo wanaosababisha ugonjwa huu wa matende nao ni,
1. Wuchereria bancrofti
2. Brugia malayi
3. Brugia timori.
Minyoo hawa huweka makazi kwenye mishipa ya limfu, hutaga mayai huzaliana kwa wingi na hivyo kuziba na kuharibu kabisa mfumo huu wa limfu. Minyoo hawa wanaaminika kuishi kwa takribani miaka 6-8 katika mwili wa binadamu.
DALILI ZA MATENDE
Maambukizi mengi huwa hayana dalili za nje lakini kwa wale ambao huonesha dalili huwa na,
1. Kuvimba mguu au miguu na kuwa na ngozi kubwa na ngumu.
2. Uvimbe ama vidonda katika sehemu husika
3. Kuvimba kwa sumbisumbi
4. Homa
5. Maumivu ya makende
6. Kupata mabusha.
Ikumbukwe kuwa baadhi ya dalili ama vionyeahi husababishwa na kinga ya mwili inapokuwa ikibambana na vimelea hawa. Miongoni mwa dalili hizi huonekana kwenye ngozi.
MATIBABU BINAFSI
1. Kwanza jikinge na aina zote za mbu ili kuzuia maambukizi mapya.
2. Fanya usafi wa mguu au sehemu husika kwa maji safi na sabuni
3. Kuufanyisha mazoezi mguu ambao unashida.
MATIBABU YA MATENDE
Matende hutibiwa kwa dawa za minyoo ambazo hutolewa hospitalini. Iwapo hutaona dalili zozote fika hospitali mapema ili kupata matibabu.
Via Dr.Emmanuel
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!