FAHAMU KUHUSU WATOTO WANAOZALIWA NA MENO
MENO
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU WATOTO WANAOZALIWA NA MENO.
Kitendo cha kuzaliwa na meno kimekuwa kikitafsiriwa tofauti katika jamii zetu. Baadhi ya jamii wanaambatanisha na baraka huku wengine wakihusianisha na laana au bahati mbaya.
Baadhi ya meno yanaweza kuwa yamekomaa, mengine yanaweza kuwa yamelegea na baadhi yanakuwa yanaonekana kuwa ndo yanataka kuota.
Mtoto kuzaliwa na meno sio kitu cha ajabu kama wengi wanavyokitafsiri. Inasadikika kuwa tukio hili hupata mtoto 1 kati ya watoto 2000-30000 wanaozaliwa.
Mara nyingi watoto hao uzaliwa na jino moja au mawili na mara nyingi huota katika taya la chini.
SABABU.
1. Kurithi
2. Matatizo ya vichochea(hormones) kwa mama kama hormone zinazotengenezwa na tezi ya pituitary na thyroid.
3. Kuongezeka kwa ufanyaji kazi wa seli zinazotengeneza meno na mifupa.
4. Maambukizi ambayo mtoto anapokea kutoka kwa mama awapo tumboni kama kaswende yanaongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye meno.
5. Upungufu wa vitamini ambayo inaweza sababishwa na upungufu au ukosefu wa chakula kwa mama mjamzito, kifafa nk
6. Homa wakati wa mimba
7. Iwapo vishimo vinavyotakiwa meno kuota vitakuwa juu juu vinapelekea kuongezeka kwa uwezekano wa kazaa mtoto mwenye meno.
8. Baadhi ya magonjwa.
MADHARA YA MENO HAYO KWA WATOTO NA MAMA.
1. Inaweza pelekea mtoto kulivuta lile jino wakati akipumua na hivyo kulifanya jino hilo lituame kwenye mirija ya upumuaji au kwenye mapafu na hivyo kuleta shida ya upumuaji.
2. Inaweza pelekea mchubuko au mchaniko mdogo kwenye ulimi wa mtoto hali inayoweza sababisha kidonda kwenye ulimi.
3. Shida katika kunyonya au kukataa kunyonya kabisa.
4. Mchubuko kwenye titi/ziwa la mama.
MATIBABU.
Iwapo mtoto amezaliwa na meno ni vyema ukatoa taarifa kwa daktari aliekaribu na wewe. Yeye ndiye atakae amua kumtoa jino au kuliacha kutokana na atakavyoona. Mzazi huruhusiwi kumng’oa jino jau meno.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!