FAHAMU KWA KINA TATIZO LA KUVIMBA MISHIPA YA TUMBO(CAPUT MEDUSAE)

FAHAMU TATIZO LA KUVIMBA MISHIPA YA TUMBO(CAPUT MEDUSAE)

• • • • • •

Caput medusae ni tatizo linaloambatana na kutokea kwa mishipa ya damu iliyovimba kwenye tumbo,mara nyingi huwa haina maumivu yoyote. Huwa ni dalili kubwa ya uwepo wa matatizo fulani ya INI kwa mhusika.


Uwepo wa shinikizo la juu ya damu kwenye mishipa inayobeba damu kutoka kwenye utumbo mdogo,tezi za nyongo na pancrease (Portal hypertension) kwenda kwenye ini huwa ndiyo sababu kubwa ya kutokea kwa tatizo hili. Kwa nyakati chache sana linaweza pia kusababishwa na kuziba kwa mrija mkuu wa inferior vena cava unaobeba damu kutoka sehemu za chini ya mwili kwenda kwenye moyo. Watu wanaopatwa na changamoto hii wanapaswa kufika hospitalini haraka,daktari atakuchunguza na ikibidi atakufanyia vipimo vya CT scan au Ultrasound ili kuthibitisha pasipo shaka uwepo wa tatizo hili. Baada ya hapo utapatiwa matibabu! cr.afyainfo 

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!