FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU ALLERGY(MZIO)

FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU ALLERGY(MZIO)

➡️ Allergy


🔻NINI MAANA YA ALEJI?

Mzio au aleji (allergy) ni matokeo ya mpambano uliopitiliza kati ya kinga ya mwili na kitu chochote (ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili) inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.

.

.

🔻HUSABABISHWA NA NINI?

Kwa kawaida kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali hatari kwa afya kama vile vimelea vya bakteria na virusi, lakini wakati mwingine inaweza kupambana pia na vitu ambavyo havina madhara yeyote kwa mwili (ambavyo huitwa allergens) na kutengeneza kemikali mbalimbali ikiwemo histamine ambayo hupambana na allergens hizo. Watu wenye aleji/mzio huwa na hisia zisizo za kawaida za mwili dhidi ya baadhi ya vitu.


Baadhi ya visababishi (allergens) ni pamoja na vumbi vumbi, baadhi ya dawa, baadhi ya vyakula, kung'atwa na wadudu kama vile nyuki, aina fulani ya uyoga, vumbi vumbi la maua (pollens) n.k.

.

.

🔻DALILI 

1•Kama ni mfumo wa hewa ndiyo ulioguswa, mtu anaweza kuwa na matatizo katika kupumua (kikohozi au kubanwa na pumzi, makamasi na kuziba kwa pua, muwasho kwenye pua na koo, au kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi)

2•Kama macho yataguswa, muhusika hujihisi hali ya kuchoma choma, kutiririkwa na machozi na muwasho kwenye macho, macho kuvimba na kuwa mekundu

3•Iwapo mtu atakula kitu ambacho ana aleji nacho anaweza kuwa na dalili kama vile kuharisha, kichefuchefu, kutapika, Kusokotwa au kuumwa na tumbo.

4•Allergens zinazogusa ngozi zinaweza kusababisha ngozi kuwa na mabaka mabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kuota vipele na malengelenge, michubuko au ngozi kuwa nyekundu.

.

.

🔻NI KWELI ALEJI INATIBIKA?

Njia bora kabisa ya kutibu na kupunguza uwezekano wa kupata aleji ni kutambua kitu au vitu vinavyokusababishia hali hiyo na kuviepuka. 

Zipo aina mbalimbali za dawa zitumikazo kutibu na kuzuia aleji. Dawa hizi ni pamoja na za jamii ya antihistamines, za jamii ya corticosteroids ambazo ni maalum kwa kutuliza mcharuko mwili (inflammation)

.

.

MUHIMU

Kama ni dawa, jitahidi kukwepa aina hiyo ya dawa, acha matumizi yake na pia mueleze daktari wako au muuguzi kabla hajakupatia dawa hizo pindi unapokwenda hospitali kwa matibabu ya matatizo mengine.


 #drtareeq

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!