FAHAMU KWA UNDANI TATIZO LA KELOIDS

FAHAMU KWA UNDANI TATIZO LA KELOIDS

➡️ KELOIDS

Mambo zenu wote,leo napenda nidokeze kwa ufupi tatizo liitwalo KELOIDS(Kiswahili chake halisi sikipati vizuri laini wat umara nyingi huita makovu makubwa,manundu,vivimbe vya kuumia nk). Hii ni tatizo ambalo Ngozi inakua na uoto au kutokea na viuvimbe ama  vijinundu vidogo n ahata makubwa na hali hii hutokea kwenye ngozi  baada ya aidha KUUNGUA,KUUMIA ama wa silaha yeyote kama panga,risasi,wembe na hata kujiumiza kwa kujikuna na kucha tu.HII HALI HUTOKEA KWA BINADAMU TU HAITOKEI KWA MNYAMA YEYOTE YULE.Ili upate shida hii ni lazima kuwe na JERAHA wenye Ngozi.

Sasa kama tunavyojua unapopata jeraha kwenye Ngozi kunakua na utaratibu wa kupona na kutengeneza kovu ,SASA WATU WANAOPATA KELOIDS HUA WANALUNDIKA KWA KIASI KIKUBWA VITU AMBAVYO MWILI HUTUMIA PALE INAPOREKEBISHA PALIPOUMIA(COLLAGENS) NA KUSHINDWA KUISHEPU UPYA BAADA YA KUPONA.Huku kushindwa huku kunaacha sehemu iloumia kua na hayo makovu makubwa ama uvimbe huo na hua UNASAMBAA MBALI NA ENEO LENYE JERAHA.NA HUPENDA SANA KUTOKEA MAENE YA USONI,KIFUANI,MABEGANI,SHINGONI NK

Hili tatizo linawapata Zaidi WATU WEUSI,WANAWAKE  NA KAMA KUNA MTU WENYE FAMILIA ALISHAPATA HIO HALI.

Hali hii ni ENDELEVU NA HUA HAIISHI NA NI NGUMU SANA KUTIBU mpaka leo.unapotokewa na hali hii usihangaie kukikata mwenyewe,au kukiminya kwani kufanya hivo kunapelekea KUKUA KWA KASI NA KUA KIKUBWA ZAIDI.

Waweza pata dalili kama mvuto kwenye Ngozi,maumivu au kuwashwa laini hua haina shida nyingine tofauti na UREMBO AU MUONEKANO Na hivi vikitokea sehemu za siri vinaweza kuharibu kabisa maumbile na muo 




JUA YAFUATAYO ILI USAIDIE WENGINE
1. HUU SIO UCHAWI:dada zangu na jamii yote usimlaumu MAMA FLANI AU KUMNYOOSHEA KIDOLE cha uchawi pale anapokutoga sikio ili uweke herein na badala yake linaanza kuvimba.hajasababisha yeye bali mwili wako ndo uko hivo.ACHA FIKRA ZA USHIRIKINA NA KUGOMBANA NA HAO KINA MAMA/DADA
2. USIKIBINYE/KUKIKATA:ukifanya hivo hautakua umejisaidia bali ndo unaongeza tatizo.ukiona hakikufurahishi nenda hospitali ili USAIDIWE.Zipo dawa za kusaidia kuzipunguza,kuondoa miwasho nk
3. KUEPUKA;Njia pekee ya kuepuka keloids ni kuepuka kupata JERAHA kwenye Ngozi.utaepuka kwa kukwepa upasuaji au ufanyiwe upasuaji pale inapobidi,kukwepa kujikwangua kwenye Ngozi na kucha,kuacha kunyoa nywele na vitu vyenye ncha kali kama wembe nk,kuacha kutoga masikio nk.SAS HAYA NLOYASEMA NI YA KUZINGATIA HASA HASA WALE WENYE HISTORIA YA HILI TATIZO KWENYE FAMILIA ZAO.
4. USAFI.Unapopata maambukizi kwenye kidonda ni chanzo kingine ambacho huweza kupelekea kupata hii shida.zingatia usafi sana.
5. Kama kuna Rafiki yako,ndugu yako,mpenzi wako,mme wako au mke wako mwenye hii shida,TUSIWATENGE,TUSIWANYANYAPE BALI TUWAPENDE NA KUWAPA USHIRIKIANO WOTE ILI NAO WAISHI MAISHA YENYE RAHA KAMA WEWE.
#doktamathew



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!


0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!