FAHAMU KWIKWI NA MATIBABU YAKE

KWIKWI

• • • • • •

FAHAMU KWIKWI NA MATIBABU YAKE.


Kwikwi ni kitendo kisicho cha hiari kinachosababishwa na kusinyaa kwa misuli ya upumuaji(diaphragm) ikifuatiwa na kufunga kwa kisanduku ya sauti(vocal cords)


Kwikwi inaweza kumtokea mtu yeyote na mara nyingi hudumu kwa muda mfupi. Iwapo kwikwi yako itadumu kwa zaidi ya masaa 48 tafadhari muone daktari. Kwikwi ya muda mrefu inapelekea -ukosefu wa usingizi

-msongi wa mawazo

-kuchoka


VISABABISHI VYA KWIKWI.

Zipo sababu nyingi sana zinazopelekea mtu kupata kwikwi baadhi yake ni,

1. Vyakula vya moto ambavyo huketa kero kwenye mshipa wa fahamu(phrenic nerve) ambao upo karibu na koo la chakula

2. Kuwepo kwa gesi ndani ya tumbo inayopelekea kusukumwa kwa misuli ya upumuaji (diaphragm)

3. Kula haraka haraka na kula kupita kiasi(kuvimbiwa)

4. Kunywa vitu vyenye gesi (carbonated drinks) kama soda na vinywaji vingine vyenye kaboni.

5. Baadhi ya madawa

6. Matatizo ya tumbo/ mfumo wa chakula kama kukwama kwa chakula ndani ya utumbo mwembamba na kucheuwa kwa chakula kwa mtu mzima.

7. Unywaji wa pombe uliopitiliza

8. Majuto, furaha iliyopitiliza , mshutuko

9. Matatizo ya ini na figo

10. Pumu na homa ya mapafu(pneumonia) 

11. Ajari katika kichwa au magonjwa yahusuyo mfumo wa fahamu

12. Uvimbe kwenye ubongo au shingoni kama lovu(goiter)

13. Magonjwa au maambukizi ya koo la hewa

13. Kula vyakula vyenye viungo vingi

14. Upungufu wa maji na madini mwilini.


MATIBABU YA KWIKWI.

Kwikwi sio ugonjwa ila inaweza ikawa ni dalili ya tatizo jingine mwilini. Iwapo kwikwi itadumu muone daktari. 

Matibabu ya kwikwi iliyodumu kwa muda mrefu au ambayo inamsumbua sana mtu ni dawa ambazo hutolewa hospital mara baada ya kugundua chanzo cha tatizo. Zipo njia nyingi(njia mbadala) za kutibu kwikwi uwapo mazingira ya nyumbani. Zifuatazo ni baadhi tu ya njia za kutibu au kuzuia kwikwi ya kawaida.

1. Kwa mtoto mchanga anaenyonya muweke begani kumfanya acheuwe hii huondoa kwikwi.

Kwa mtu mzima fanya hivi;

1. Kunywa maji ya baridi sana taratibu au kwa kugugumia.

2. Bana pumzi ndani kwa muda mfupi kisha toa hewa nje rudia *3au 4

3. Jitapikishe kwa kidole

4. Kunywa kiasi kidogo cha SIK(vinegar)

5. Vuta na kutoa pumzi kwenye karatasi yenye umbo la boxsi inayofunika uso.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!