FAHAMU MADHARA YA UFUPI KWA MWANAMKE WAKATI WA KUJIFUNGUA

 YAPI NI MADHARA YA UFUPI KWA MWANAMKE WAKATI WA KUJIFUNGUA?

đź—ŁTafiti Zinaonyesha mwanamke ambaye ni mfupi mfano chini ya CM 150.Yupo kwenye hatari ya kujifungua kwa upasuaji ikilinganishwa na mwanamke ambaye yupo kwenye urefu wa juu ya CM 150.

Ufupi huathiri Njia ya mtoto atakayopitia ikiwemo Mfupa wa kiuno ambapo kitaalam hujulikana kama PELVIC BONE kuwa mwembamba na kumbana mtoto,hivo kumzuia mtoto kupita kwa Njia ya kawaida.

Japo sio kila mwanamke Mfupi basi atajifungua kwa Upasuaji,ila hii pia ni mojawapo wa vihatarishi vya mwanamke kujifungua kwa Njia ya kupasuliwa.

Kama wewe ni mfwatiliaji wa mambo au Mchunguzi,moja ya vitu ambayo mwanamke akiwa mjamzito hupimwa ni Urefu,hivo utaona katika kadi la Kliniki la mama pale juu wameweka tiki kama Urefu wake upo chini ya Cm 150 au Juu ya Cm 150.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!