FAHAMU SABABU KUBWA ZA MAZIWA YA MWANAMKE KULALA

MAZIWA KULALA

• • • • • •

FAHAMU SABABU KUBWA ZA MAZIWA YA MWANAMKE KULALA


Vipo vitu vingi ambavyo huchangia mabadiliko ya  umbo la titi la Mwanamke,ambapo baadhi ya sababu ni za mda mfupi na zingine ni za mda mrefu.


SABABU ZA MAZIWA YA MWANAMKE KULALA


✓ Kwa asilimia kubwa Mama akishabeba ujauzito tu,umbo la titi huanza kubadilika na kuwa kubwa na wakati mwingine kushuka


✓ Kujifungua Mara nyingi pamoja na kuwa na watoto wengi


✓ Uvutaji wa sigara kwa mwanamke,nayo pia ni miongoni mwa sababu zinazochangia maziwa ya mwanamke kulala


✓ Kadri umri unavyosogea ndivo na umbo au shape ya Maziwa hubadilika na kushuka


✓ Kuwa Mnene kupita kiasi kunaweza kusababisha matiti yako kushuka


✓  Lakini pia kwa wengine,hii hali hutokana na kuwepo kwa vinasaba vya hali hii katika ukoo wao hivo ni kama tatizo la Kurithi.


✓ Upungufu mkubwa wa baadhi ya Vitamin Mwilini Mfano VITAMIN C.  Hii ni kutokana na Kuwa Vitamin C hutengeneza kitu kinachoitwa COLLAGEN ambacho ni muhimu sana katika kuimarisha ngozi ya Ziwa pamoja na kushikilia ziwa lisishuke. Hivo basi upungu wa Vitamin C ni upungufu wa Collagen na ni matokeo ya Ziwa kushuka.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!