VIFO+WAJAWAZITO
• • • • • •
FAHAMU SABABU KUBWA ZINAZOPELEKEA VIFO VYA KINA MAMA WAJAWAZITO.
Imani zetu kama wanadamu ni kwamba kuzaliwa na kufa ni mipango ya mwenyezi Mungu. Lakini kwa upande wa afya inaaminika kuwa baadhi ya vifo vinaweza kudhuirika iwapo hatua sitahiki zitachukuliwa.
Kampeni mbalimbali zinaendelea nchini ili kupunguza au kutokomeza kabisa tatizo la vifo vya kina mama wajawazito. Lakin ili hili litimie ni jukumu la watoaji wa huduma ya afya, wanajamii na kina mama wajawazito wote kushiriki katika zoezi hili.
Asilimia kubwa ya vifo hivi vinaweza kuzuilika kabisa.
MIONGONI MWA SABABU ZA MOJA KWA MOJA ZIPELEKEAZO VIFO KWA KINA MAMA WAJAWAZITO NI:
1. Kutokwa na damu nyingi wakati wa mimba au mara baada ya kujifungua.
2. Shinikizo la damu litokanalo na mimba na kifafa cha mimba.
3. Uzazi pingamizi
4. Maambukizi wakati wa mimba au baada ya kujifungua
5. Utoaji mimba usio salama.
SABABU ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA NI:
1. Upungufu wa damu
2. Malaria
3. Maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Mama mjamzito unashauriwa sana kuenda kliniki na kuwa na maudhurio mazuri kliniki kwani matatizo mengi hugundulika wakati wa kliniki.
By Emmanuel Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!