FAHAMU SABABU ZINAZOPELEKEA KUZAA WATOTO WENYE KASORO WAKATI WA KUZALIWA PAMOJA NA JINSI YA KUZUIA.

WATOTO

• • • • • •

FAHAMU SABABU ZINAZOPELEKEA KUZAA WATOTO  WENYE KASORO WAKATI WA KUZALIWA PAMOJA NA JINSI YA KUZUIA.


Kasoro wakati wa kuzaliwa huunganisha kasoro zote za kimaumbile (kiumbo), kitabia, akili, kazi na kimetaboliki. 3% y watoto wanaozaliwa huwa na kasoro hizi. 

Kasoro hizi ni kama kichwa kikubwa, kichwa kidogo, upungufu wa akili, uono hafifu, usikivu hafifu au kutokuona kabisa, mdomo sungura, mguu kifundo, mgongo waza n.k


Kasoro nyingi hutokea wakati wa utengenezwaji wa sehemu mbali mbali za mwili (organ) na mara nyingi hutokea kati ya wiki ya 3-8 mara baada ya mimba kutungwa. 

Kasoro hizi huusisha kutokuwepo, kuwepo kwa baadhi au kubadilika kwa mpangilio wa sehemu flani ya mwili. Kasoro ndogo ndogo ni kama kuzaa mtoto mwenye masikio madogo akiwa na madoa madoa n.k na mara nyingi kasoro hizi hazina madhara.


SABABU ZINAZOPELEKEA KUZAA MTOTO AMBAYE TAYARI ANA  KASORO WAKATI WA KUZALIWA.

 Sababu hizi zimegawanywankatika makunfi matatu nayo ni,

1. Kimazingira

2. Urithi

3. Mwingiliano wa kurithi na mazingira. 

Na hizi ndizo sababu kwa ujumla

1. Maambukizi ya virusi kama rubella, cytomegalovirus n.k virus hawa huweza kupita kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni na hivyo kuleta shida kwa mtoto.

2. Mionzi- mionzi huuwa seli na hivyo kulingana na dozi yake huweza kupelekea aina yoyote ya kasoro 

3. Joto kubwa mwilini litokanalo na homa au kitu kitoacho joto kama mashine.

4. Dawa- kama dawa zitumikazo kutibu degedege, magonjwa ya akili sonono, msongo wa mawazo  na kutuliza maumivu. Mfano wa dawa ni (thalidomide, valproic acid, lithium, lead n.k) MAMA MJAMZITO USITUMIE DAWA YOYOTE PASIPO USHAURI WA DAKATARI.

5. Kisukari wakati wa ujauzito

6. Uzito uliopitiliza

7. Upungufu wa oksijeni wakati wa mimba

8. Upungufu wa madini na vitamini wakati wa mimba

9. Matumizi ya bangi, tumbaku, sigara, pombe na madawa mengine ya kulevya wakati wa mimba.

10. Matumizi ya dawa zenye vichocheo

11. Dawa aina ya DES.


JINSI YA KUZUIA.

1. Uandaaji na upikaji mzuri wa vyakula kama nyama.

2. Kutokugusana na kinyesi cha wanyama kama paka.

3. Kutumia chumvi yenye iodine.

4. Kudhibiti sukari wakati wa mimba

5. Kutumia folic acid wakati wa mimba

6. Kutokutumia pombe, na sigara.

By Emma




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!