FAHAMU UNDANI KUHUSU NYAMA NYEKUNDU

Nyama nyekundu kwa lugha rahisi kabisa ni ile nyama ambayo kabla ya kupikwa huwa na muonekano wa rangi nyekundu. Mfano ni nyama ya ng’ombe,kondoo na nguruwe

-

Nyama nyekundu huwa na virutubisho muhimu sana kwa afya ya binadamu hasa vitamin B3,B12,B6,madini ya chuma,zinc na selenium. Huwa pia na utajiri mkubwa wa protini. Virutubisho hivi vinafaa kwa afya ya binadamu

-

Binadamu anashauriwa kutumia kiasi kisichozidi gram 70 za nyama nyekundu kila siku. Kiwango cha kawaida kwa wiki nzima kisizidi gram 500,yaani nusu kilo tu. Hapa ndipo utapata faida za nyama nyekundu,kinyume cha hapo unaweza kuhatarisha afya yako

-

Tafiti nyingi zimekuwa zinasisitiza kupunguza matumizi ya nyama nyekundu kwa kuwa huwa siyo nzuri sana kwa afya ya binadamu hasa inapotumika kwa kiasi kikubwa. Mojawapo ya machapisho haya ni lile la Feb 3,2020 kwenye jarida la Kitabibu la JAMA Internal Medicine linaloeleza uhusiano wa nyama nyekundu na saratani,kisukari pamoja na matatizo ya moyo

-

Pamoja na kuwa na faida nyingi kwa afya,nyama nyekundu hubeba kiasi kikubwa cha lehemu,kemikali zisizofaa pamoja na mabaki ya Trimethylamine N-oxide (TMAO) yanayopatikana baada ya kumeng’enywa kwa nyama hii tumboni. Hivi ndivyo vyanzo muhimu vya magonjwa ya moyo,kisukari pamoja na aina mbalimbali za saratani

-

Hukatazwi kula nyama hizi,lakini inafaa uzitumie kwa kiasi kinachoshauriwa cha 70 gram  kwa siku,au nusu kilo kwa wiki nzima ili uilinde afya yako. Athari hizi za nyama nyekundu zinathibitishwa pia na andiko la NIH’s National Heart, Lung, and Blood Institute (NHLBI),lililotolewa Sep 10,2018 kwenye jarida la kitabibu la European Heart Journal (kwa wanaohitaji references)

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!