ZIJUE FAIDA ZA CHAI YA MDALASINI
• • • • • •
Watafiti hutumia aina kuu mbili za mdalasini ambazo ni Cinnamon cassia (Cinnamomum aromaticum) pamoja na mdalasini halisi,Cinnamomum verum (Ceylon cinnamon).Katika tafiti nyingi,kazi za mdalasini husomwa bila kujali sana aina ya mdalasini uliotumika kwa maana aina zote hizi hutofautiana kidogo sana kwa viwango vya kemikali zake
-
Chai ya mdalasini huharibu sumu mwilini,huboresha afya ya moyo,hushusha presha ya damu na kuvunja mafuta yasiyofaa mwilini,hupunguza sukari mwilini hasa kwa watu walio na aina ya pili ya kisukari,huua bakteria na fangasi pamoja na kupunguza maumivu ya hedhi.Mdalasini huongeza kinga za mwili hasa kwa watu walio na VVU pamoja na saratani
-
Huandaliwa kwa kuchemshwa kwenye maji kidogo. Asali na majani ya chai ya rangi yanaweza kuongezwa ili kuboresha ladha yake.
-
Chai hii isitumike kwa kiasi kikubwa sana kwa watu wenye matatizo ya ini pamoja na wale wenye tatizo la figo. Wanawake wajawazito wanaweza kutumia mdalasini kama kiungo cha chakula,au kama chai (lakini isiwe nyingi sana).Watu walio na kisukari wanaweza kutumia huku wakiendelea na dozi ya dawa zao kama walivyoshauriwa hospitalini. cc.afyainfo
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!