FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO
UNYONYESHAJI
• • • • • •
FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA NA MTOTO.
Kunyoshesha kuna faida nyingi kwa mama na mtoto, Mtoto azaliwapo anatakiwa kunyonya maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita (6) ya kwanza bila kupewa kitu kingine chochote, hata maji.
Faida kwa mtoto.
1. Maziwa ya mama ya virutubisho vyote vihitajikavyo mwilini kwa ukuaji wa mtoto.
2. Maziwa ya mama kwa mtoto yapo katika aina ambayo inaweza kumeng'enywa kirahisi na mfumo wa umeng'enyaji wa kichanga ambao kwa wakati huo haujakomaa.
3. Maziwa ya mama yana kinga ambayo husaidia kumkinga mtoto na magonjwa mbali mbali ikiwemo bacteria na virus.
4. Tafiti zinaonesha kuwa mtoto ambae ananyonya maziwa ya mama pekee kwa miezi 6 ya kwanza ana uwezekano mdogo sana wa kupata magonjwa ya masikio (otitis media), magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama vile pneumonia, na kuharisha ukilinganisha na watoto wasionyonyeshwa au wanaopewa vyakula vingine kabla ya muda.
5. Kunyoshesha kunaongeza upendo wa mtoto kwa mama sababu ya ukaribu wao pindi anyonyeshapo.
6. KUNYONYESHA kunakuza akili ya mtoto.
Post ijayo tutaona faida za KUNYONYESHA kwa mama
Prepared by Dr Sam CEO/ founder of SAM NUTRITIONAL CLINIC
For more help Contact with us :-
(+255) 0789699225 (whatsapp/call/sms) Dr Sam 🤳👨🏻⚕️
Ukiwa umependa makala hii na ungepanda kupata elimu sahihi ya afya kila siku, usihaau kuliki ukurasa Wetu ili kutopitwa na makala zetu pendwa za afya.
Pia Unaweza kuwa mwalimu kwa wengine kwa KUS-hare makala hii zaidi na zaidi ili wengi wapate Elimu hii uliyoipata wewe.
“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako”.
.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!