FAIDA ZA MTOTO MCHANGA KUBEUA
MTOTO+KUBEUA
• • • • • •
Watoto wachanga wanaonyonya maziwa ya mama wengi hawapati tatizo la gesi kwa wingi kama watoto wanaokunywa maziwa ya kopo (baby formula) ,sababu mtoto anaponyoya kwa chupa anaingiza hewa tumboni kwa wingi na inakuja kumuumiza tumbo. Ila mtoto anaenyonya ziwa la mama ni kiasi kidogo cha hewa kinachoingia tumboni.
Watoto wanatakiwa wasaidiwe kubeuwa baada ya kunyonyeshwa. Inamsaidia; •Kutoa gesi baada ya kunyonya
•Kumwepusha na maumivu ya tumbo
•Kumwepusha kucheuwa na macheuwo kupitia puani
Mtoto anapomaliza kunyonyeshwa mweke begani ,mpige pige mgongoni taratibu kwa dakika chache mpaka umsikie amebeuwa. Epuka kumlaza kabla haja beuwa – kucheuwa baada ya kumnyonyesha sababu akicheuwa yatapitia puani na kumfanya ashindwe kupumua na kupata maumivu makali.
Muhimu umbebe kwa dakika 5-15 ndio umlaze.
#drtareeq
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!