HATUA ZA UNYWAJI WA POMBE/HATUA ZA ULEVI
ZIJUE HATUA ZA UNYWAJI WA POMBE/HATUA ZA ULEVI
Bila shaka sisi sote tunaelewa au tunajua maana ya pombe na namna zinavyonyweka. Kiburudisho hiki kina historia ya muda mrefu hapa ulimwenguni na kimeanza kunywewa hata kabla ya kuzaliwa kwa Yesu kristo wa nazareti na Mtume Mohammad S.A.W.
Pombe ni kipooza/kisononesha ubongo(depressant) na sio kichangamsha ubongo(stimulant) kama wengi mnavofahamu.
Ukimtazama kwa makini mtu anaekunywa pombe utagundua kua anakua anapitia hatua kadhaa huku akiendelea kupata kinywaji chake,na mara nyingi wengi hutafsiri kama ni furaha.
Nitenda kulezea kwa kifupi hatua 7 ziwapatazo watu wanaokunywa pombe. Hatua hizo hutofautiana baina ya mtu na mtu kutokana na sababu mbalimbali kama kiasi cha pombe ulichokunywa,uzito wa muhusika,kama umekula au la na tumboni kuna chakula kiasi gani,kiasi cha Mafuta katika chakula ulichokula,jinsia na utimamu wa mwili
HATUA HIZO NI KAMA IFUATAVYO
1) HATUA YA KWANZA NI-USOBA:Katika hatua hii mtu hua mkimya mkimya au anakua anapiga stori za kawaida tu. Katika hatua hii mtu anakua ndo anaanza kunywa pombe na mara nyingi ndo hua kwenye glass ya kwanza ya pombe. Mtu ambae yupo katika hatua hii hua na kiwango cha BAC ya 0.05 au pungufu cha pombe kwenye damu
2) HATUA YA PILI NI-RAHA;Katika hatua hii mtu huanza kujisikia furaha Zaidi,anakua anajiamini kupita maelezo,kuanza kutongoza tongoza kila mtu,anakua hana aibu,anakua muongeaji sana na mtu wa watu sana. Hatua hii hutokea kukiwa na kiasi cha pombe kwenye damu cha 0.03-0.12 BAC.
3) HATUA YA TATU NI-MSISIMKO:katika hatua hii mtu huanza kujiona mjanja mjanja na kuanza kujihisi kama amelewa au watu wanamuona amelewa. Pia katika hatua hii mtu huanza kupoteza muelekeo katika mazungumzo(kuchelewa kujibu),kutapika na kushindwa kuamua mambo. Hatua hii hutokea kukiwa na kiasi cha pombe kwenye damu cha 0.09-0.25 BAC
4) HATUA YA NNE NI-KUCHANGANYIKIWA;Hii hatua hutokeaa kama kuna kiasi cha pombe kwenye damu cha 0.18-0.30 BAC
5) HATUA YA TANO NI-STUPA;katika hatua hii mtu hua amepoteza ufahamu wake kwa kiasi kikubwa,hawezi kunyanyuka kwenye kiti,hawezi kusimama,hawezi kuongea,kutapika,kujikojolea,kujinyea nk. Mtu akifikia hapa ni lazima apate msaada wa kidaktari ndo aweze kuishi. Hatua hii hutokea kukiwa na kiasi cha pombe kwenye damu cha 0.25-0.40 BAC
6) HATUA YA SITA NI-COMA:Katika hatua hii mtu hua amezimia,amepoteza ufahamu wote na hawezi kufanya kitu chochote ikiwemo hata kupumua na kazi za moyo. Mtu akifika hapa bila msaada wa haraka wa kimatibabu basi atapoteza uhai. Hatua hii hutokea kukiwa na kiasi cha pombe kwenye damu cha 0.35-0.45 BAC
7) HATUA YA SABA NI-KUFA;kiasi cha pombe kwenye damu kikifika 0.45 BAC na kuendelea basi shughuli zote za mwili husimama na mtu atakua amepoteza uhai.
(NA Dokta mathew
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!