Ticker

6/recent/ticker-posts

HOMA YA UTI WA MGONGO(MENINGITIS),VISABABISHI VYAKE,DALILI,MADHARA NA TIBA YAKE



HOMA YA UTI WA MGONGO 

• • • • • •

Homa ya uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi.


VISABABISHI 

1•Bakteria; Beta-streptococci, Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae na Mycobacteria tuberculosis

2•Virus; Herpes simplex type 2, HIV na Varicella zoster.

3•Fangasi; Coccoidiodomycosis na Cryptococci meningetides.

.

.

DALILI NA VIASHIRIA 

1•Shingo kukakamaa na kuwa ngumu isivyo kawaida

2•Mgonjwa kujihisi homa kali

3•Maumivu makali ya kichwa

4•Mgonjwa kupoteza fahamu

5•Mgonjwa kupatwa na degedege (seizures) na mwili kukakamaa

6•Mgonjwa kushindwa kuvumilia mwanga (photophobia)

7•Mgonjwa kutoweza kukaa sehemu yenye makelele (phonophobia)

8•Kwa watoto, kuvimba utosi

.

.

MADHARA YA HOMA YA UTI WA MGONGO

.

1•Kuamshwa kwa chembechembe za damu zinazo sababisha damu kuganda kitaalamu – Disseminated Intravascular Coagulopathy (DIC).

2•Kuvuja damu kwa katika tezi za adrenalin na kupelekea kutokea kwa ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa – waterhouse friderichsen syndrome.

3•Kwa watoto, ugonjwa huu unaweza kusababisha mtoto kuwa na kichwa kikubwa - hydrocephalus.

.

.

MATIBABU 

Kwa wagonjwa waliopoteza fahamu ni vizuri kuhakikisha wanapumua vizuri, na njia za hewa ziko wazi. Halikadhalika, iwapo itathibitika kuwa bakteria ndiyo wanaosababisha ugonjwa huu, mgonjwa anaweza kupewa mojawapo ya dawa hizi za antibiotiki kama cefotaxime au Cefriaxone. Aidha baadhi ya madaktari hupendelea kuongeza dawa za steroids kama dexamethasone kama sehemu ya matibabu.


Iwapo itathibitika ugonjwa huu umesababishwa na virus, dawa kama Acyclovir huweza kutumika. Hali kadhalika, ikithibitika kuwa vimelea waliosababisha ugonjwa huu ni wa kundi la fungus, dawa kama Amphotericin B au flucytosine zaweza kutumika. Mgonjwa pia hupewa Paracetamol kwa ajili ya kushusha homa na kuondoa maumivu ya kichwa.cc.drtareeq


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!







Post a Comment

0 Comments