SARATANI
• • • • • •
IFAHAMU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI SABABU NA DALILI ZAKE.
Saratani ya shingo ya kizazi ifahamikayo kama cervical cancer ni saratani ambayo hushambulia seli(chembe chembe) zilizo katika shingo ya kizazi ya mwanamke. Saratani hii inasadikika kuwa ni miongoni mwa saratani zinaoongoza kwa vifo vya wanawake duniani. Huathiri wanawake kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea. Sababu kubwa ya saratani hii ni aina ya kirusi afahamikaye kama human papilloma virus ambaye hushambulia seli za shingo ya kizazi na kuzifanya zikuwe na kuzaliana kwa kasi sana ikiwa ni kinyume na mpangilio wa kawaida wa uzalianaji wa seli hizo.
Mara nyingi mabadiliko hutokea taratibu sana hivyo wanawake wanashauliwa kufanya vipimo mara kwa mara ili kugundua kama wanasaratan hii.
VISABABISHI/ VIHATARISHI.
1. Umri- uwezekano wa kupata saratani hii uongezeka kadri umri unavyoongezeka
2. Kurithi- kuwa na historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia
3. Maambukizi ya virusi aina ya HPV
4. Uvutaji wa tumbaku/ sigara
5. Kukutana kimwili na mwanaume katika umri mdogo
6. Kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja
7. Kukutana kimwili na mwanaume ambaye hajatahiriwa
8. Hali duni ya kiuchumi
9. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa na upungufu wa kinga mwilini
10. Matumizi ya dawa za kupanga uzazi kwa muda mrefu
11. Idadi kubwa ya nzao( yaani watoto wengi)
DALILI
Katika hatua za walai za ugonjwa huu dalili huwa hazionekani lakini kadri saratani inavyokuwa dalili hutokea. Baadhi ya dalili ni,
1. Kutoka damu sehemu za siri zaidi ya mzunguko wa kawaida wa mwezi
2. Kutoka majimaji au uchafu wenye harufu mbaya sehemu za siri
3. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
4. Maumivu ya mgongo
5. Kuvimba miguu
6. Kupingua uzito (kukonda)
NB: kuna chanjo ambayo hupewa wanawake ili kuzuia maambukizi ya HPV na hivyo kuzuia saratani hii. Chanjo hii kwa Tanzania imeanza kutolewa kwa mabinti kati ya miaka 9-14.
Via Emmanuel Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!