Pembe tatu ya kifo kwenye uso wako: Wengine wanaita Danger triangle of the face au Triangle of Death. Eneo hili linazunguka pembe za mdomo na pua, Ni eneo hatari sana ambalo makosa madogo yanaweza kukusababishia kifo au maambukizi mengine kwenye ubongo. Kutokana na uwepo wa mkusanyiko wa mishipa mingi ya damu inayoenda puani na maeneo ya pembeni yake kuna uwezekano mkubwa endapo mtu atapata maambukizi eneo hili, aidha kutokana na ngozi kuchanika/kupasuka au njia nyingine yoyote, maambukizi haya yanaweza kufika kwenye ubongo.
-
Usipende kukuna au kutumbua kila upele unaotokea katika eneo hili, Kumbuka ni eneo lenye mishipa mikubwa ya fahamu minne (four major cranial nerves) ambazo hufanya kazi usoni. Moja ya shida ambazo utaweza kupata endapo utasumbua mfumo huu ni kupooza (paralysis) au uvimbe mkubwa.
-
Kwa wale mnaopenda kutoa nywele puani inabidi aidha muache hii tabia au muongeze umakini. Msitumie mafuta au dawa zozote za kupata ili kuondoa nywele za puani. Lakini kumbuka pia vinyweleo hivi vina kazi muhimu sana katika uvutaji wako wa hewa mwilini.
(📝 @festongadaya )
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!