IJUE SARATANI YA KOO,WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA,DALILI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 SARATANI YA KOO


Hii ni saratani ambayo hutokea eneo la koo,na pia huhusisha mfumo mzima wa mmeng'enyo wa chakula kuanzia kwenye koo mpaka mwisho tumbo linapoanzia.


Zamani saratani ya koo ilikuwa inawapata sana watu wazima,ila kwa hivi sasa saratani ya koo huwapata hata Vijana wadogo kabsa.


SABABU ZA KUPATA SARATANI YA KOO


Zipo sababu nyingi zinazochangia mtu kupata saratani ya Koo ikiwemo;


1. Matumizi ya tumbaku na Uvutaji wa Sigara


2. Unywaji wa baadhi ya pombe zenye kemikali kali au unywaji wa pombe kupindukia


3. Kuwa na umri mkubwa hasa kuanzia miaka 65 na kuendelea


4. Kuwa na matatizo ya tumbo ambayo huhusisha acid kurudi kutoka tumboni kupanda juu kwenye koo yaani ACID REFLUX kwa kitaalam.


5. Athari za tindikali au acid kutokana na tatizo Sugu la kucheua Tindikali pia ni chanzo kikubwa cha Saratani ya koo


6. Unene kupita kiasi huweza kuchangia pia Saratani ya koo


DALILI ZA SARATANI YA KOO


dalili za Saratani ya koo ni pamoja na;


- Mtu kushindwa kumeza mate

- Mgonjwa kushindwa kumeza chakula

- Mgonjwa kupata maumivu makali wakati wa kumeza kitu

- Maumivu ya kifua na Mgongo

- Kupatwa na shida ya kiuungulia

- Kupungua uzito kwa kasi

- Kupatwa na shida ya Sauti kukwaruza


MATIBABU


Saratani hii hutibika kabsa endapo,itagundulika mapema kabsa ya kufika stage mbaya.

Yapo matibabu mengi yakiwemo yale yanayohusisha Mionzi.


Kwa Ushauri zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!