Ili mmeng'enyo wa chakula ufanyike vizuri huhitaji mambo mengi sana na miongoni mwa mambo hayo ni kujishughulisha kwa mhusika katika kufanya kazi yoyote inayohitaji matumizi ya nguvu (physical activities).Wakati wa asubuhi na mchana,watu wengi huwa wapo busy katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku,haijalishi ni aina gani ya kazi unafanya,ile tu kuwa busy kidogo (hata kutembea tu) huusaidia sana mfumo wa mmeng'enyo wa chakula katika kumeng'enya na kuzitumia vizuri nguvu zinazozalishwa kupitia mlo huo.
-
Tofauti na ilivyo kwa mlo wa usiku,watu wengi sana wamezoea kupata chakula hiki dakika chache tu kabla hawajaenda kulala.Hii ni mbaya sana na pamoja na uwepo wa athari zingine,kuongezeka kwa uzito wa mwili na uwepo wa tatizo la kupatwa na choo kigumu huwasumbua sana watu.Unapokula chakula na kwenda kulala,miondoko ya misuli ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hupungua sana hivyo kufanya chakula hiki kirundikane tumboni kwa muda mrefu,pia nguvu zinazozalishwa na chakula hiki huwa haziunguzwi kikamilifu.Usipokuwa unasumbuliwa na choo kigumu bila shaka tatizo la kuongezeka sana kwa uzito wa mwili litakukabili
-
Jitahidi upate mlo huu saa mbili hadi tatu kabla hujaenda kulala.Pilikapilika zozote zile bila kujalisha zinatumia nguvu kiasi gani ni muhimu sana katika kusaidia mmeng'enyo wa chakula chako.Hata kama utaamua kufanya mazoezi magumu kiasi gani,bila kubadili ratiba yako ya mlo wa usiku itakuwa ni ngumu sana kwako kuupata uzito unaouhitaji!
Cr: @hosymichael
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!