IJUE SIRI YA MAFUTA YA MGANDO(PETROLEUM JELLY)

MAFUTA MGANDO (Petroleum Jelly) yapo sokoni kwa zaidi ya karne moja na nusu; yameendelea kuaminiwa na madaktari bingwa wa ngozi kama mafuta rafiki kwa ngozi hasa kwa watu wenye shida za ngozi kama mzio, vidonda nk.


Mafuta ya mgando hutengeneza mazingira wezeshi ambayo huchochea vidonda hasa michubuko kupona haraka.Hupunguza uwezekano wa maambukizi kwenye vidonda vidogo kwenye ngozi.


Mafuta mgando husaidia afya ya ngozi na kupunguza dalili mbaya za magonjwa yatokanayo na mzio wa ngozi kama pumu ya ngozi na magonjwa mengine kama psoriasis.Hupunguza uwezekano wa kupata muwasho wa ngozi.


Mafuta mgando husaidia kupunguza mzio wa ngozi kwa watoto

Mzio wa ngozi husababisha ngozi za watoto kuwasha na kutoka mapele.Mgando huweza kutumika kwa mtoto kuanzia wiki 3. Mafuta mgando husaidia kuilinda ngozi ya mtoto dhidi ya vipele vya pampers (diaper rash) ambavyo husababishwa na mikojo/kinyesi kuathiri ngozi.Mafuta mgando hayana kemikali zaidi hivyo huwa rafiki kwa ngozi.


Mafuta mgando husaidia kupunguza maumivu kwa mtu mwenye bawasiri (hemorrhoid).Bawasiri huweza kusababisha maumvu wakati wa haja kubwa, mafuta ya mgando husaidia kupunguza hali hiyo.


Yalitengenezwa mara ya kwanza kusaidia vidonda kupona


Matumizi yaliongezeka hadi

-Kuzuia pua zisikauke hivyo kuzuia damu kutoka puani

-Kupunguza vipele sehemu za Siri visivyo magonjwa ya zinaa

-Kusaidia uponaji fangasi wa kucha nk


MUHIMU

Mafuta mgango hayafai kuwa kilainishi wakati wa kufanya mapenzi kwani huweza kuongeza uwezekano wa Kondomu kupasuka. Pia huongeza uwezekano kwa wanawake kuugua magonjwa ya uke hasa bacterial vaginosis.Cc.afyainfo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!