UTI
• • • • • •
U.T.I ni maambukizi katika njia ya mkojo na huathiri mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi, wadudu huathiri sana kibofu na urethra.
✍🏻Jina U.T.I ni kifupi cha URINARY TRACT INFECTION (Neno la kingereza) watu wengi huzoea kuita hivyo wakijua ni jina la kiswahili, imeshazoeleka hivyo. Jinsia ya kike wana hatari kubwa kuliko jinsia ya kiume.
✍🏻Maambukizi yakwenye kibofu huleta maumivu makali, madhara makubwa hutokea maambukizi yakifika mpaka kwenye figo. U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo.
✍🏻U.T.I hutibika haraka kwa mtu ambaye atatumia dawa na pia yaweza kuleta madhara makubwa isipotibika huweza kuathiri mfumo wa uzazi, kibofu, na sehemu mbalimbali, tunashauri mtu mwenye U.T.I inatakiwa awe msafi na kubadili mienendo iliyo hatarini.
MGAWANYO WA UGONJWA WA U.T.I
✍🏻Kuna mgawanyo wa aina mbili za U.T.I
➡️Maambukizi ya Upande wa juu. Hii hujumuisha Figo na Ureta
➡️Maambukizi ya Upande wa chini. Hii hujumuisha Kibofu na Urethra
CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA U.T.I
✍🏻U.T.I husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo, mazingira yafuatayo yanaweza kukuingiza kwenye hatari ya kupata U.T.I;
➡️Kinga ya mwili kuto kuwa imara
➡️Kutumia Vifaa au Dawa za kuzuia mimba
Kwa wa kike; Kupungua kwa homoni ya estrogeni
➡️Mtu mwenye kisukari
➡️Kutumia choo kichafu na kutumia idadi kubwa ya watu
➡️Kuwa na tatizo la mmeng’enyo na tatizo la choo
➡️Kukaa kwa mda mrefu bila kutembeatembea
Prepared by Dr Sam CEO/ founder of SAM afyakwanza
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!