Ticker

6/recent/ticker-posts

JANGA LA CORONA,MAANA YA KIRUSI HIKI,DALILI ZAKE,JINSI UNAVYOSAMBAA,TIBA YAKE



CORONA

• • • • • •

JE, NI KIRUSI GANI HIKI?

Ni kirusi kipya kabisa. Coronavirus, ni familia kubwa ya virusi, lakini ni aina sita pekee vinavyojulikana kuwaambukiza watu.


Mfano, Kirusi cha SARS kinachosababishwa na Coronavirus, kiliwaua watu 774 kati ya 8098 walioambukizwa katika mlipuko wa ugonjwa huo ulioanza China 2002.

.

.

DALILI ZAKE NI ZIPI?

Huonekana kuanza na vipimo vya juu vya joto mwilini na kufuatiwa na kikohozi kikavu na baada ya wiki moja, kinasababisha tatizo la kupumua huku wagonjwa wakihitaji usaidizi wa hospitali.  Kirusi cha Corona chenyewe kinaweza kusababisha homa mbaya itakaoendelea hadi mgonjwa kupoteza maisha yake.

.

.

JE VIRUSI HIVYO VINATOKA WAPI?

Vinaelezwa kutokana na mnyama, lakini bado hajafahamika na mamlaka zinasema muda tu eneo linalohifadhi wanyama ambapo virusi hivyo vinapatikana litakapotambuliwa , tatizo hilo litakuwa rahisi kutatua.


Watafiti wanasema kwamba virusi vipya vinahusishwa kwa ukaribu na vile vilivyopatikana katika popo. Hatahivyo hatua hiyo haimanishi kwamba popo wa msituni ndio waliosababisha mlipuko huo

.

.

UNASAMBAAJE BAINA YA WATU?

Mwanzo wa mlipuko, mamlaka za China ilisema kwamba virusi hivyo havisambai kupitia mtu mmoja hadi mwingine, lakini sasa visa kama hivyo vimetambuliwa.


Wanasayansi sasa wamefichua kwamba kila mtu aliyeambukizwa anawaambukiza kati ya watu 1.4 na 2.5.

.

.

JE KUNA CHANJO AMA TIBA YOYOTE?

Hakuna...

Hatahivyo mpango wa kutengeneza chanjo unaendelea.


Ni matumaini kwamba utafiti kuhusu kutengeneza chanjo ya virusi vya Mers ambavyo pia ni virusi vya Corona itafanya kazi kuwa rahisi.


Na hospitali zinafanyia majaribio dawa za kukabiliana na virusi vya ukimwi kuona iwapo zina athari yoyote kwa waathiriwa.


Mchanganyiko wa dawa mbili - Lopinavir na Ritonavir - ulifanikiwa dhidi ya ugonjwa wa Sars na inafanyiwa majaribio nchini China wakati huu wa mlipuko huu mpya.

.

.

CHA KUFANYA

1. Kuzuia ziara za watu.

2. Kuosha mikono mara kwa mara

3. Kuwatibu wagonjwa katika maeneo yaliotengwa kwa kuvaa vifaa vinavyozuia maambukizi hayo.

Cc.drtareeq

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!







Post a Comment

0 Comments