JE INACHUKUA MDA GANI KUPATA MTOTO AU MIMBA BAADA YA WANANDOA KUOANA?

JE INACHUKUA MDA GANI KUPATA MTOTO AU MIMBA BAADA YA WANANDOA KUOANA?

Kuna WANAWAKE/WANAUME/WANANDOA hudhan  na hu plan wakioana tu fasta WATAPATA MIMBA na MTOTO.

Ni Rahis sana kwa baadhi ya Couple/wanandoa(hulifanikisha hivyo hivyo).

Lakin Sasa sio kila wanandoa Hufanikisha Hili/hubarikiwa hili.

Utafiti unasema hivi,wanandoa wanaangukia kati ya nafasi HIZI TATU


1.asilimia 25(25%) ya wanandoa hufanikiwa Kupata MIMBA wakikutana Mwezi mmoja tu,anapanga kabisa ni siku za hatar aki sex kwel anapata MIMBA,hawa ni gusa unase.


2.asilimia 50(50%) idadi kubwa zaidi ya wanandoa hufanikiwa MIMBA ndani ya MIEZI sita.


3.Jumla,ina general asilimia 85 mpaka 90(85%-90%) mwaka Unapoisha wanakuwa wamepata Mimba.


4.asilimia 10 mpaka 15(10-15),unaisha mwaka wanakuwa hawajafanikiwa,na hapa ndipo TUNASHAURI UCHUNGUZI na TIBA kwa hawa wanandoa.


Wanandoa msipopata mimba ndani miezi MICHACHE(mwanamke aliechini ya miaka 35),relax,zingatien ushauri wa namna ya kupata mimba naturally,yaan hapa ni mambo ya LISHE,kunywa folic acid,mazoezi,kuacha  pombe/sigara(Nilipost TIPS za kusaidia KUPATA MIMBA nadhan mliona wengi) 


Unakuta mtu kaolewa,kakosa mimba MIEZI MIWILI TU,ananitafuta analia anataka vipimo na TIBA.


Mwanamke ulie chini ya miaka 35,Kama inapita  MIEZI 12 yaan MWAKA bila mafanikio ndipo UCHUNGUZI ZAID unashauriwa.(kwa wanawake wenye miaka zaid ya 35  ikipita miezi 6 haujapata MIMBA  unatakiwa Kutuona wataalamu kwa ushauri,Uchunguzi na Tiba).


Wewe unaangukia kwenye kundi Lipi kati ya HAPO?????


đź“ŚNB kwa wanandoa ambao mnatafuta mimba/mtoto MJE WOTE  yaan kwa PAMOJA kwenye vituo vyetu vta kutolewa huduma ilishauriwe kwa pamoja,mchunguzwe kwa pamoja na kutibiwa kwa pamoja kama kuna ULAZIMA..


Wanaume acheni imani potofu ya kuona wanawake ndo wanamatizo na pekee ndo wanahitaji kuchunguzwa  na kutibiwa(SIKU HIZI WANAUME WENGI SANA WANASHIDA YA UZAZI)


Unakuta mwanamke kanywa madawa MIAKA HATA MIWILI(Hata kama kaambiwa Hana shida yeyote,anakunywa tu masikin) lakin sasa mwanaume wake Hajawah hata Kumuona Daktari na ka Relax kabisaaaaa hana Habari(nadhan Ipo kwenye mfumo dume SANA,tunaendelea kulisema na kulipigia Kelele ONE DAY YES,patakaa sawa hapa).

Cc: Uzazipoint #afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!