JE NI WAKATI GANI MWANAMKE ANATAKIWA KUSEMA KAPATA HEDHI KUPITA KIASI?
HEDHI
• • • • • •
Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi..!!!
⭐Unapata hedhi inayozidi siku 7
⭐Unapata hedhi nzito inayofanya ubadiri pedi moja ndani ya masaa mawili
⭐Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuvaa pedi zaidi ya moja
⭐Unapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje
⭐Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi
⭐Hedhi inayotoka na mabonge
Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi;
👉Viuvimbe kwenye kuta za mji wa kizazi; vivimbe hivi sio saratani huitwa fibroids
Yai kupevuka bila mpangilio (Irregular ovulation) ; hali hii husababisha kuta za mji wa mimba zivimbe na kuwa nene hivyo kutoa damu nyingi. Hutokea zaidi kipindi cha kuvunja ungo na kipindi cha kukaribia ukomo wa hedhi
👉Matumizi ya dawa za kuzuia damu kuganda
👉Baadhi ya wanawake waliotumia vitanzi (IUD) hasa ndani ya mwaka wa kwanza
👉Maambukizi ya mji wa mimba na mirija ya uzazi (PID)
👉Endometriosis
👉Saratani ya mji wa kizazi; kwa kinamama waliofikia umri wa ukomo wa hedhi. Wakianza kupata hedhi isiyokoma huweza kuwa dalili ya saratani ya mji wa kizazi.
Ukiwa umependa makala hii na ungepanda kupata elimu sahihi ya afya kila siku, usihaau kuliki ukurasa Wetu ili kutopitwa na makala zetu pendwa za afya.
Pia Unaweza kuwa mwalimu kwa wengine kwa KUS-hare makala hii zaidi na zaidi ili wengi wapate Elimu hii uliyoipata wewe.
“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!