JE ULAJI WA NYAMA YA NGURUWE UNA MADHARA?

NYAMA YA NGURUWE

• • • • • •

Hata kiwango kidogo cha nyama nyekundu na nyama iliyosindikwa kama kipande cha nyama ya nguruwe iliyokaushwa kwa siku kinaweza kuongeza hatari ya kansa ya utumbo, kwa mujibu wa utafiti.


Utafiti wa hivi karibuni wa Chuo kikuu cha Oxford uliodhaminiwa na taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza, unaongezea ushahidi kuthibitisha hayo, pia ule uliotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kwamba ulaji wa nyama nyekundu unaweza kuwa na madhara.


KILE UTAFITI ULICHOBAINI:

Watafiti walitathmini data kutoka kwa watu wapatao nusu milioni waliohusika katika utafiti uliofanywa na kituo cha Uingereza cha utafiti wa kibaiolojia -UK Biobank


Kwa zaidi ya miaka sita ya uchunguzi wao walibaini watu 2,609 walipata kansa ya utumbo.


WALIKADIRIA:

1. Ulaji wa vipande 3 vidogo vya nyama ya nguruwe kila siku badala ya kula mara moja tu unaweza kusababisha kuongezeka kwa hatari ya kansa ya utumbo kwa asilimia 20


2. Kwa kila watu 10,000 katika uchunguzi huo walikula gramu 21 za nyama nyekundu na za kusindikwa, 40 kati yao walipatikana na kansa ya utumbo.


NI KIWANGO GANI CHA ULAJI WA NYAMA NI KIKUBWA KUPITA KIASI?

Haijawa wazi. Taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza -Cancer Research UK (CRUK) inasema visa 5,400 kati ya visa 41,804 vya saratani ya utumbo vinavyopatikana nchini Uingereza vinaweza kuzuiwa kama watu hawali nyama za kusindikwa kabisa


NI SAWA KULA NYAMA KIDOGO?

Muongozo wa taasisi ya NHS unasema kuna baadhi ya faida za nyama nyekundu zina madini ya chuma na protini. Watu wanaweza kula nyama na bado wakawa wenye afya.


NI NINI KINACHOSABABISHA HATARI?

Nyama za kusindikwa -zikiwemo za nguruwe, baadhi ya soseji, hot dog-hubadilishwa kwa kiasi kwamba zinaweza kukaa kwa muda mrefu. Njia kuu ni kuzichoma, kuzitibu au kuziongezea chumvi au kuziwekea kemikali za kuzuia zisioze.


Pia kemikali zinazohusika katika usindikaji zinaweza kuongeza hatari ya saratani. Viwango vya juu vya joto vinavyotumia katika kupika.


Kwa suala la nyama nyekundu kama nyama ya ng'ombe, kondoo na nguruwe, kuna madai kuwa moja ya protini inayosabisha nyama hizo kuwa nyekundu inaweza kuharibu utumbo.


Lakini wataalamu bado wanaendelea kujaribu kuelewa zaidi madai hayo.

via.drtareeq




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!