JE ULTRASOUND INADANGANYA JINSIA YA MTOTO?

ULTRASOUND

• • • • • •

JIBU: Shida siyo ultrasound,shida ni yule anayeitumia ultrasound


Ultrasound machine yaani Kifaa ni OPERATOR DEPENDANT MACHINE,yaani yenyewe inaonesha tu,shida ni kama msomaji hayupo vizuri kuchanganua anachokiona. Mashine haina shida kabisa bali shida ni yule anaekupiga picha pale na uelewa wake,utaalamu wake pamoja na uzoefu wake.

-

Ndio maana kama Mpiga picha Sio mtaalamu sana kwenye hili,Anatakiwa AEPUKE Kutaja jinsia za watoto kuepuka kuleta Shida kama hizi

-

Na ndio maana sehemu nyingi hawakuambii jinsia kabisa kuepuka hili,kuna wanawake wanahisi hata wamebadilishiwa watoto kumbe shida ni yule aliempiga picha.

-

Uwezo wa wapiga picha umetofautiana sana,kuna mwenye diploma,mwenye degree na mwenye masters (yaan ni specialist, BINGWA) hawa ni watu watatu tofauti kabisa,lakini pia Kuna uzoefu. Hivyo,Inategemea unafanya wapi ultrasound na ni nani anakupiga.

-

Unapoambiwa JINSIA usichukulie asilimia 100 ndugu,wakati mwingine mfano,mpiga picha anaweza ona Korodani za mtoto akajua ni Mashavu Ya uke akakuambia ni mtoto wa kike

-

Kuwen makini sana na hili swala la kuangalia Jinsia. Unaweza kuambiwa jinsia fulani kisha ukakutana na jinsia tofauti ikakuathiri kisaikolojia pamoja na malezi ya mtoto. Mtoto ni wako,subiri afike miezi 9 ukabidhiwe ndipo ujue jinsia!

(đź“ťCredits: @uzazipoint )




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!