JE UNAYAJUA MADHARA YA KUCHOKONOA MENO KWA STICK?

 JE UNAYAJUA MADHARA YA KUCHOKONOA MENO KWA STICK?

➡️ Meno


Watu Wengi sana wana Desturi ya kuchokonoa Meno kwa Stick mara tu baada ya kula Vyakula Mbalimbali kama Nyama au matunda yenye asili ya kamba kamba kama Maembe,machunga n.k

Lengo kuu,likiwa ni kutoa uchafu kwenye Meno, Njia hii sio salama kiafya.

Tabia ya kuchokonoa meno mara kwa Mara kwa kutumia Stick husababisha uwepo wa Majeraha ya Fizi,Fizi kutoa Damu au kuweka shimo katika shina la Jino,hivo kutengeneza mazingira ya bacteria kukaa hapo na kuanza kula Jino taratibu taratibu

Matokeo ya tabia hii,ni mtu kupata ugonjwa wa kuumwa na Meno,pamoja na matatizo ya Fizi zako.


🔻KIPI KIFANYIKE?

Njia salamaa ya Kusafisha meno au kutoa Uchafu kwenye Meno yako ni kwa Kupiga mswaki mara tu baada ya kula Chakula chochote.

Epuka Tabia hii ya kuchokonoa meno yako kwa kutumia Stick mara kwa mara,kwani sio Salama katika afya ya Meno

.

.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!